Vyama vya Kiislamu vinavyoiunga mkono rasimu ya katiba mpya vimepata ushindi katika awamu ya kwanza ya kura ya maoni juu ya rasimu hiyo, lakini upinzani umedai kuwepo kwa udanganyifu na kuitisha maandamano siku hapo kesho.
Kwa mujibu wa chama cha Haki na Uhuru ( Justice and Freedom) ambacho ni tawi la kisiasa la chama cha udugu wa Kiislamu asilimia 56.5 walipiga kura ya Ndio.
Wapinzani wamesema hawatayatambua matokeo hayo hadi yajumulishwe na matokeo ya awamu ya pili, itakayofanyika Jumamosi ijayo.
Makundi ya uangalizi wa zoezi hilo yamedai kulikuwepo na kasoro nyingi, zikiwemo ukosefu wa majaji katika baadhi ya vituo vya kupigia kura, na wanawake kuzuiwa kupiga kura katika baadhi ya vituo.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Misri amesema malalamiko yote juu ya zoezi hilo yatachunguzwa na kufanyiwa kazi.
Post a Comment