Ripoti ya Umoja wa
mataifa iliyofichuliwa inasema wanajeshi kutoka Rwanda walihusika moja kwa moja
na utekaji wa mji wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliotekelezwa
na waasi.
Ripoti hiyo
iliyokusanywa kwa ajili ya baraza la usalama, inasema wanajeshi mia tano wa
Rwanda, walihusika katika utekaji huo wa kundi la M23.
Wanajeshi wa Congo
walirudi Goma hapo jana siku mbili baada ya waasi kuondoka kutoka mji huo wa
Goma mwishoni mwa wiki baada ya mkataba wa amani uliofikiwa kwa usaidizi wa nchi
za ukanda wa Maziwa Makuu.Msemaji mmoja wa jeshi la Rwanda ameiambia BBC kuwa
tuhuma hizo ni za kuudhi na zisizo na msingi.
Lakini waasi wameonya
kuwa watauteka tena mji huo ikiwa serikali haitatimiza matakwa yao katika muda
wa siku mbili.
Waasi hao waliondoka
Goma siku kumi na moja baada ya kuuteka mji huo kutoka kwa wanajeshi wa DRC
wakiungwa mkono na wanajeshi wa amani wa Umoja wa Mataifa
Mnamo Jumatatu mamia ya
wanajeshi wa DRC waliwasili katika kambi zao mjini Goma baada ya waasi kuondoka
kutoka mji huo mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini siku ya
Jumamosi.
Uwanja wa ndege wa mji
huo utafunguliwa Alhamisi ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingizwa huko
kuwasaidia mamia ya watu walioachwa bila makao baada ya kutoroka
mapigano.
Waasi hao walikubali
kusonga umbali wa kilomita 20 kutoka Goma ikiwa serikali itatimiza matakwa yao
ikiwemo kuwaachilia wafungwa wa kisiasa. Lakini duru zinseama kuwa wangali wako
karibu sana na mji wenyewe kinyume na makubaliano walioafia.
Kuna hofu kuwa hatua yao
isidumu ikiwa Rais Joseph Kabila atakataa kuanza mazungumzo nao kulingana na
msemaji wa waasi hao kanali Vianney Kazarama
Post a Comment