 |
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA DIWANI |
 |
MAREHEMU
JOSEPH MWASOKWA
MNAMO TAREHE 09/12/2012
MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO MAENEO YA BLOCK - T JIJI NA MKOA WA MBEYA. JOSEPH
S/O NELSON MWASOKWA, MIAKA 78,KYUSA, AFISA USALAMA WA TAIFA MKOA WA MBEYA
[MSTAAFU] NA MKAZI WA BLOCK T . ALIGUNDULIWA KUUAWA NYUMBANI KWAKE KWA KUKATWA
NA KITU CHENYE MAKALI KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA SEHEMU ZA SHINGONI, KICHWANI
MABEGANI NA MKONO WA KUSHOTO. KATIKA TUKIO HILO HAKUNA KITU CHOCHOTE CHA
MAREHEMU KILICHOCHUKULIWA KWANI MAREHEMU ALIKUTWA NA PESA TASLIMU TSHS 107,000/=
DOLA 200 ZA KIMAREKANI NA SIMU MOJA YA MKONONI. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA
WAKATI AKIINGIA KWENYE GETI LA NYUMBA YAKE. KWA MARA YA MWISHO MAREHEMU ALIRUDI
NYUMBANI NA JIRANI YAKE MAJIRA YA SAA 20:00HRS TOKA SOWETO KUTAZAMA FAINALI YA
MPIRA WA MIGUU KOMBE LA CHALLENGE KATI YA UGANDA NA KENYA. CHANZO CHA MAUAJI
HAYO BADO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA
NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE.
Signed
By,
[DIWANI ATHUMANI –
ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
|
on Monday, December 10, 2012
Post a Comment