Mwezeshaji wa mafunzo ya siku
tatu kwa waandishi wa Habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika
utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC), Balozi
Jeremy Ndayiziga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo yaliyoliyoanza
leo Jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi kutoka nchi Wanachama wa EAC.
Kulia ni Mtaalam wa Masuala ya Habari kutoka EAC, Sukhdev Chhatbar, ambaye pia
ni mratibu wa mafunzo hayo. Balozi Ndayiziga ni Mtaalam katika Masuala ya
Mtengamano wa EAC.
Washiriki wakichangia mada katika mafunzo hayo
ambayo yameandaliwa kwa pamoja kati ya EAC na Shirika la Kijerumani la GIZ.
Washiriki wakifuatilia mada na michango ya
washiriki wengine kwa umakini.
Mwandishi Mkongwe, Zephania Ubwani kutoka Mwananchi
Communication Ltd, Arusha akichangia mada. Kulia ni Salma Saidi pia wa Mwananchi
na DW Zanzibar.
Picha ya pamoja ya washiriki wote na
wawezeshaji.
Mtaalam wa Masuala ya Habari
kutoka EAC, Sukhdev Chhatbar, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo akijadili
jambo na Mwanahabari Mkongwe na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa za Afrika,
Jenerali Ulimwengu. Ulimwengu pia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo.
Mkufunzi akiendelea na kutoa mada. Kulia ni
Mkufunzi Mwenzake Jenerali Ulimwengu akimsikiliza kwa makani na kushoto ni
Mshiriki Mwandishi Kimeli arap Kemei kutoka Kenya.
Huu ulikuwa wakati wa Mtengamano kati ya Fiona na
James
Mercy na Fiona wakiwa mkutanoni
















Post a Comment