Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda
akiwahutubia wananchi wa kata ya Nsenkwa baada ya uzinduzi wa Zahanati
ya Kijiji hicho kilichopo Mkoani Katavi ambako yupo kwa Ziara ya
kikazi.Wanachi hao walimshukuru Waziri Mkuu kwa kuwezesha kupatikana kwa
huduma ya afya ya uhakika kwani ilikuwa ni kero ya muda mrefu.Waziri
Mkuu yupo jimboni kwake ambapo yeye ni mbunge wa jimbo la Katavi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Katavi,Kamishina Msaidizi wa Polisi,Dhahiri Kidavashari akiwataka
wananchi wa kata ya Ugala kushirikiana na Jeshi la Polisi katika
kutokomeza uhalifu.ambapo alitoa namba zake za simu ikiwa ni ishara ya
kuonyesha jinsi Jeshi la Polisi linavyo himiza ulinzi shirikishi wakati
alipokuwa akiongea katika ziara ya Waziri Mkuu jimbo la Katavi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda
akionyesha jinsi ya kupalilia katika shamba la Mkuu wa Mkoa wa
Katavi,Dkt. Rajabu Rutengwe.Mh. Pinda amewataka watendeji wa Serekali
kuwa mfano kwa wananchi katika kilimo cha kutumia utalamu,alisema hayo
baada ya kuona shamba hilo lilivyo pandwa kwakuzingatia kanuni bora ya
kilimo.Picha na Chris Mfinanga.
Post a Comment