Mafanikio yaliyopatikana hivi karibuni katika vita dhidi ya Malaria yanaweza kuanza kudorora kwa sababu ya kukwama kwa ufadhili kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Katika Ripoti yake ya hivi karibuni ya Malaria Duniani imeonyesha kuwa maisha milioni 1.1 yaliokolewa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita lakini upatikanaji wafedha 2004 – 09 ulikwama 2010-12.
Pungufu ya kiasi cha Dola za marekani bilioni 1.5 zilizokuwa zikihitajika ndio kilitumika kwaka jana.
Takwimu mpya za WHO kwa mwaka 2010 zinaonyesha kuwa watu milioni 219 waliambukizwa Malaria huku watu 660,000 wakipoteza maisha.
Post a Comment