WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema wilaya mpya ya Mlele mkoani
Katavi
itakuwa
na Halmashauri mbili za Mlele na Nsimbo ili kurahisisha
utoaji
huduma
kwa wananchi.
Ametoa
kauli hiyo janamchana (Jumamosi, Desemba 15, 2012), wakati
akizungumza na wakazi wa kata ya Inyonga kwenye viwanja vya shule ya
msingi Inyonga akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake jimboni kwake
Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.

Aliwaeleza
wakazi hao kwamba Rais Jakaya Kikwete aliamua kuwapa wilaya
mpya na mkoa mpya kwa ili kuleta maendeleo kwa haraka. “Rais Kikwete
alifanya hivyo kwa sababu alijua kwamba rasilmali zikiletwa Rukwa
(mkoa wa zamani) hadi zifike hapa Mlele zitakuwa ni kidogo sana,”
alisema.

Kufuatia
mgawanyo huo, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele itakuwa na kata
13 ambazo ni Ilunde, Ilela, Nsenkwa, Inyonga, Utende, Kasanga na
Mamba. Nyingine ni Majimoto, Mwamapuli, Mbede, Usevya, Itenka na
Kibaoni.

Nayo
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo itakuwa na kata 11 ambazo ni
Ugalla, Uruira, Kasokola, Mtapenda, Nsimbo na Sitalike. Nyingine ni
Kapalala, Machimboni, Litapunga, Itenka na Magamba.

Ili
kuendana na kasi ya mabadiliko, Waziri Mkuu aliwataka wakazi
hao
wachangamkie fursa zilizopo kwa kuachana na kilimo cha matuta.
Aliwataka mabwana shamba waandae mashamba-darasa kwa kila kijiji ili
wananchi waweze kujifunza kwa mifano.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu ameahidi kutoa miche 1,000 ya miembe ya
kisasa kwa vijana wa vijiji vya Uruira na Usense wilayani Mlele kama
njia ya kuwahamasisha walime mazao mbadala.

Alitoa
ahadi hiyo jana jioni (Jumamosi, Desemba 15, 2012), wakati
akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo kwenye viwanja vya shule ya
msingi Uruira katika kata ya Uruira wakati akiwa njiani kurejea Mpanda
mjini.

“Nimemwambia
Mkuu wa Mkoa (Dk. Rajab Rutengwe) ahamasishe kilimo cha
maembe ya kisasa… yale ni makubwa ili muachane na haya madogo ya
kwenu. Vijana hawa wapeni eneo nami nitawaletea miche 1,000 ya maembe
ya kisasa kwa kuanzia,” alisema.

Akihimiza
kanuni bora za kilimo, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo
la Mlele aliwataka waachane na kilimo cha matuta na badala yake
watumie kilimo cha sesa. “Ekari moja ya mahindi inapaswa iwe na miche
16,000 ili ikupatie magunia 20-25 ya mahindi, sasa wewe unalima ekari
tatu na kuvuna magunia 10, sababu kubwa ni nafasi zinazopotea kwenye
miraba ya matuta, alisema.

“Ni
lazima tuondokane na kilimo hiki kwa sababu hakina tija na
tena
kinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo lingetumika
kupanda mazao,” alisisitiza.

Kesho
(Jumatatu, Desemba 17, 2012) Waziri Mkuu atakwenda kata za
Machimboni na Nsimbo ambako atahutubia wananchi.

Post a Comment