Miaka kadhaa imepita baada ya Kenya kukumbwa na
balaa la machafuko yaliyopelekea vifo vingi vya watu, majeraha ya kudumu na watu
wengi kukosa makazi yao baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 (post election
violence). Wasanii wa maigizo nchini humo wameshafanya filamu inayohusu matukio
yaliyotokea wakati huo na filamu inaitwa "Something Necessary". Katika filamu
hiyo wamemtumia character mmoja mwanamke aitwae Anne ambae anaonesha maisha yake
yalivyokuwa baada ya machafuko yaliyoivuruga nchi hiyo mwaka 2007, Anne ni
mwanamke anaehangaika kuyarudisha maisha yake aliyokuwa nayo kabla ya machafuko
hayo, akijaribu kupambana kwa ajili ya afya ya mtoto wake wa kiume, alipompoteza
mumewe, na shamba lake. Lakini pia yumo character mwenye jina la Joseph, yeye ni
gang member aliyehusika katika machafuko hayo, lakini wote Joseph na Anne
wanajikuta wakiwa katika wakati mgumu wakitafuta jinsi ya kuzifuta kumbukumbu
hizo mbaya na kuendelea na maisha yao ya kawaida. Iangalie trailer yake hapa,
"Something Necessary"..
on Saturday, January 12, 2013
Post a Comment