Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alifanya ziara ya ghafla
kulikagua jengo la mikutano la Chachani Chake Chake Pemba, hapa
alikuwa
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Canal Mstaafu Juma Kassim
Tindwa, jinsi ya kulinusuru jengo hilo.
Jukwaa la ukumbi wa Mikutano
wa Chachani chake, lililokuwa
likitumiwa na waheshimiwa kwa mikutano na Vikao
sambamba na burudani, ambalo kwa sasa limekuwa makazi ya
mchwa.
Hii ni hali halisi ya eneo la
ndani ya ukumbi maarufu wa mikutano uliopo Chachani Chake Chake Pemba, ambao
awali ukumbi huo ulikuwa ni jengo maalum la sinema.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akitembelea kukagua kwa nje ya jengo la ukumbi
wa mikutano la Chachani Chake Chake Pemba, ambalo liko katika hali
mbaya.Mpiga picha Hassan Issa-
OMPR-ZNZ






Post a Comment