Waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya mpanda
*************
Baraza la madiwani la
Halmashauri ya mji wa mpanda mkoa wa Katavi limepitisha uamuzi wa
kuitisha kikao maalumu cha daraza hilo ili kujadili tuhuma zinazo
ikaibili Halmashauri hiyo inayo husuana na miradi mbambali ikiwemo ghama
ya matengenezo ya shangingi la mkurugenzi wa mji huo lililo fanyiwa
matengenezo kwa ghama ya shilingi milioni 40.
Uamuzi wa kuitishwa kwa
kikao maalumu cha Baraza la madiwani ulipitishwa na Baraza hilo katika
kikao chake kilicho fanyika desemda 31mwaka jana katika ukumbi wa chuo kikuu
huria cha mkoa wa Katavi.
Taarifa ya kufanyika kwa
kikao hicho ilitolewa hapo jana na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa mpanda
Enock Gwambasa alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake.
Alisema katika kikao
kilicho fanyika desemba 31 mwaka jana Baraza hilo lilishindwa kujadili
taarifa ya kamati ya madiwami iliyo kuwa imepewa jukumu la kufuatilia huma
za miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri yake ambayo ilikuwa na
utata.
Uamuzi wa wakuitishwa
kwa baraza maalumu la madiwani umezingatia ukubwa wa wa swala lenyewe la
huhuma za ubadilifu wa fedha ambapo taarifa ya kamati ya madiwani wameisha
kamilisha taarifa hiyo yenye kurasa 22 ili madiwani waweze kuipitia kwa kina na
kuijadili.
Alifafanua kuwa
kutokana na hari hiyo Baraza la madiwani waliamua kupitisha uamuzi wa
kuitishwa kwa kikao maalumu cha baraza la madiwani ndani ya siku 14 baada ya
kikao hicho cha desemba 31 mwaka jana.
Gwambasa alizitaja
baadhi ya tuhuma za ubadilifu wa fedha ni malipo ya ya matengenezo ya
gari la mkurungenzi wa Halmashauri hiyo lenye namba STK5142 aina ya
shangingi lililo ghalimu matengenezo ya shilingi milioni 40 matengenezo
yaliyo fanyika katika gereji inayoitwa LWICHEya mjini Sumbawanga mkoani
Rukwa.
Katika malipo ya
matengenezo hayo yanayo lalamikiwa kuwa ni makubwa mkurugenzi wa Halmashauri
ya mji wa mpanda Joseph Mchina ana daiwa aliidhinisha kulipwa kwa shilingi
milioni 25 za awali kwa mwenye gereji hiyo kinyume na utaratibu wa mamlaka
aliyo nayo kama mkurungenzi ambapo mamlaka aliyo nayo yana mpa madaraka ya
kuidhinisha malipo yanayo ishi shilingi milioni 10 tuu.
Alieleza kuwa malipo
yoyote yanayo zidi shilingi milioni 10 ni lazima yaidhinishwe na kamati ya
fedha na mipango utaratibu ambao hakufuatwa katika malipo
hayo.
Gwambasa alizitaja huma
nyingine zinazo ikabili halmashauri ya mji ni mradi wa ng’ombe wa wananchi wa
kijiji cha Kakese ambapo halmashauri iliidhinisha wanunuliwe ng’ombe wakubwa
lakini inadaiwa wamenunuliwa ndama kwa bei ya ng’ombe wakubwa pamoja na mradi
wa ufugaji wa nguruwe katika ya kawajense.
Alitaja tuhuma nyingine
kuwa madai ya ujenzi wa ghara la kuifadhia chakula katika kata ya Kakese
linalo daiwa kujengwa chini ya kiwango.
Post a Comment