Mwenyekiti
wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la
Singida mjini Mh.Mohammed Gullam Dewji.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Vijana
katika halmashauri ya manispaa ya Singida wameshauriwa kufanya utafiti
wa kina juu ya faida na hasara ya ushiriki wa maandamano yanayoitishwa
na watu au viongozi mbalimbali wakiwemo wa siasa, kabla ya kushiriki.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida Hamisi Nguli
wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vyenye
thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 ilivyotolewa bure na mbunge wa jimbo
la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji.
Ameisema
kwa kawaida, kijana yeyote huwa amejawa na matengemeo na matarajio
mengi kupindukia akilini mwake na kitendo hicho ni rahisi mno
kudanganyika.
Amesema
hivi sasa wapinzani wanalielewa hilo na ndio maana wameelekeza nguvu
zao zote kwa vijana kuwadanganya kwa vile wanajua ni rahisi kuingia
mkenge.
Ameongeza
kuwa angalia maandamano y oyote utakuta vijana ni asilimia 99, na
ukiwauliza nini kilichowapeleka kuandamana na kuacha kazi za kuwaingizia
kipato halali, wanakuwa hawana jibu la maana.
Kwa
hali hiyo, Nguli amewataka vijana kuwa makini sana na maandamano kwa
madai kuwa yanasababisha hasara nyingi ikiwemo vilema vya kudumu na
wakati mwingine vifo.
Nguli amewataka vijana kutulia na kuchapa kazi halali kwa bidii na kujielimisha kwa kadri ya uwezo wao utakavyowaruhusu.
on Wednesday, January 23, 2013
Post a Comment