Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DC WA BUNDA ATUHUMIWA KWA RUSHWA


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Bunda, jana imemkamata raia wa China, Mark Wang Wei, akitoa rushwa ya Sh 500,000 kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe(pichani), ili kampuni yake iruhusiwe kusambaza pembejeo kwa wakulima, gazeti la Mtanzania limeandika

Wei, ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Panda International Co. LTD ya mkoani Shinyanga, alikamatwa jana mchana katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, baada ya mkuu huyo wa wilaya kuweka mtego.

Akisimulia tukio hilo, DC Mirumbe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Bunda, alisema Mchina huyo kupitia kampuni yake ambayo ni ya usambazaji wa pembejeo, juzi alimwandikia ujumbe wa simu ya kiganjani akimshukuru na kuahidi kumuona jana ofisini kwake, ili ampe zawadi yake.

Alisema baada ya kuahidiwa na Mchina huyo, hali hiyo ilimtia shaka, kwani hakuwa na ahadi yoyote kutoka kwake, na ndipo akaamua kuwataarifu TAKUKURU ambao waliweka mtego.

“Baada ya kuahidiwa, hali hiyo ilinishtua na kunitia wasiwasi, nilichokifanya niliona ni vyema kumtaarifu mkuu wa PCCB ili aweke mtego,” alisema. Alisema Mchina huyo, alifika jana mchana na kuingia ofisini kwake na kumpa barua kutoka Idara ya Uhamiaji, ikimtambulisha kuwa anacho kibali cha kuishi nchini hadi Machi mwaka huu.

Alisema baada ya kukabidhiwa barua hiyo, bila wasiwasi Mchina huyo alitoa Sh 500,000 na kumkabidhi na kusisitiza kuwa ni zawadi yake kwa ajili ya kuisaidia kampuni yake iweze kusambaza pembejeo kwa wakulima.

Alisema suala la usambazaji wa pembejeo, linatakiwa kusimamiwa na mtu makini, kwani msimu uliopita mawakala waliopewa jukumu hilo walichakachua pembejeo na kusababisha wakulima kutozipata kwa muda muafaka.

Alisema kufuatia hali hiyo, baadhi ya watendaji wa hamashauri hiyo walioshirikiana na mawakala hao wamesimamishwa kazi na wengine wameshitakiwa mahakamani.

Alisema hali hiyo ndiyo iliyowasukuma kuwa makini katika suala zima la kupitisha mawakala wa kusambaza pembejeo wilayani hapa, ambapo walibaini kuwa Mchina huyo alikuwa na kibali cha kumruhusu kuishi nchini ambacho muda wake umebaki siku 10 tu.

“Kampuni yangu iliomba tenda ya kusambaza pembejeo wilayani Bunda, siku ya mkutano sikuwepo, kwa hiyo nimekuja na zawadi hii ili nimpe DC…hii si rushwa ni zawadi tu,” alisema.

Alipoulizwa ni zawaidi ya nini, alisisitiza ni kwa sababu ya urafiki tu kwa sababu China na Tanzania zina urafiki wa siku nyingi na hakujua kama ni kosa.

Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bunda, Masuke Ogwa alisema kampuni ya Mchina huyo ilikuwa haijaruhusiwa kusambaza pembejeo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top