Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DKT. KIGODA AKEMEA UFISADI UJENZI

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda ameziagiza halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji nchini kufuatilia gharama za ujenzi wa miradi katika maeneo yao, akisema kuna wizi mkubwa unafanyika katika kandarasi hizo.
Alisema miradi mingi hasa ya ujenzi imekuwa ikichakachuliwa sana na makandarasi pamoja na baadhi ya wataalamu wanaosimamia miradi hiyo, kwa kupandisha gharama kubwa ilhali mradi wenyewe ni wa bei ya kawaida. Akisema hali hiyo isipodhibitiwa haraka inatishia uchumi wa taifa.
Wito huo aliutoa juzi wakati akifungua mradi mpya wa mnada wa mifugo, katika Mji mdogo wa Mkata uliopo katika Tarafa ya Mazingara, wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.
Dk Kigoda ambaye pia ni Mbunge wa Handeni amewaagiza wasimamizi wa maendeleo katika maeneo hayo wakiwemo wakurugenzi, wenyeviti, pamoja na wakuu wa wilaya, kudhibiti wizi unaofanywa katika zabuni hizo.
“Miradi mingi ya ujenzi inachakachuliwa sana, inasomwa gharama kubwa ya ujenzi, lakini unakuta mradi kama ule umejengwa kwa gharama ndogo zaidi. Miradi mingi haiendani na gharama halisi, wengi wanajali masilahi binafsi,” alisema Dk Kigoda na kuongeza.
“Mfano mzuri ni mradi wa Bwawa la Kijiji cha Suwa hapa Handeni, limegharimu kiasi cha Sh90 hadi 120 milioni, lakini bwawa kama hilo kuna kijiji kimeingia mkataba na mkandarasi kwa takribani Sh295 milioni, huo ni wizi mkubwa ambao hatutauvumilia,” alisema.
Hata hivyo Dk Kigoda amepongeza uongozi wa halmashauri hiyo hasa Kamati ya Uchumi kwa kuweza kuanzisha miradi mikubwa ya maendeleo ukiwemo wa Kituo cha Mabasi cha Segera.
Dk Kigoda ameagiza halmashauri hiyo kuchimba kisima kirefu cha maji katika eneo hilo la mnada ili kuweza kuwa na uhakika wa kupata maji wakati wote ukilinganisha na Mradi wa maji wa Handeni Trank Man (HTM) ambao unahitaji ukarabati mkubwa.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Hassan Mwachibuzi alimweleza waziri huyo kwamba mnada huo uliojengwa pembezoni mwa Barabara kuu ya Segera-Chalinze umegharimu Sh87 milioni.
Alisema lengo la kuanzishwa kwa mnada huo ni kuimarisha mapato ya halmashauri pamoja na kuwakomboa wafugaji kutoka katika vijiji vilivyopo kwenye Tarafa za Kwamsisi, Mazingara na Magamba, ambapo jumla ya Ng’ombe 50,000 pamoja na mbuzi 90,000 wanatarajiwa kuuzwa katika mnada huo utakaofanyika kila siku ya Jumatano.
Alisema kwamba ujenzi wake ulianza mwaka 2010. Ulichelewa kukamilika kutokana na kumtimua mkandarasi waliompa awali kwa vile alijenga chini ya kiwango.
Mwachibuzi amewataka wafugaji kutumia fursa hiyo, kuvuna sehemu ya mifugo yao kwenda kuiuza mnadani hapo, ili kujipatia fedha kwa ajili ya maendeleo yao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top