Waziri Mkuu Mhe. Mizengo
Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya wadau mbalimbali wa mkoa huo
ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi
asilia.
Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
Taarifa mpya zitawekwa
hapa punde zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza rekodi ya kipindi cha
Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia muhtasari wa yaliyojiri katika kikao
cha jana kati ya Waziri Mkuu na Wadau.
UPDATES/TAARIFA MPYA ZA ZIARA YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu alikuwa
akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani
wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha
wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi
kesho.
Dondoo muhimu:
Dondoo muhimu:
- Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar
- Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye
- Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa.
- Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
- Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar
- Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu
- Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa)
- Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa
- Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu
Post a Comment