Mwaka mpya wa 2013
umekaribishwa kwa aina yake duniani kote,wakati mamilioni ya watu wakimiminika
katika bandari ya mjini Sydney nchini Australia,eneo la sherehe mjini Berlin na
mjini London kuangalia fashifashi.
Baadhi ya watu
waliokusanyika kusherehekea walijikusanya katika maeneo tulivu , wakivalia
mavazi nadhifu ya kimono ama kula vyakula wavipendavyo.
Pia kulikuwa na
tukio lililozoeleka la kuweka tufe la dunia katika uwanja wa Times mjini New
York , sherehe ambazo zilichafuliwa na kifo mwaka jana cha Dirk Clark , mshauri
maalum wa muziki wa rock ambaye kwa miaka kadha amekuwa akisimamia sherehe hizo
katika televisheni moja ya Marekani licha ya kuathirika na ulemavu
uliosababishwa na ugonjwa wa kiharusi.
Fashifashi zikirushwa
angani kuukaribisha mwaka mpya mjini Berlin.
Mjini Berlin
Mjini
Berlin , mamia kwa maelfu ya watu waliokuwa wakifurahia waliunganisha mikono yao
katika mitaa iliyojaa watu katika juhudi zao za kutaka kuvunja rekodi ya dunia
kwa kucheza midundo ya muziki maarufu wa Gangnam style, uliopigwa na mwanamuziki
kutoka Korea ya kusini kwa muziki wa kufoka foka Psy. Gangnam , na wachezaji hao
walicheza kwa kufuatia mirindimo ya kuhesabu dakika kuelekea mwaka
mpya.
Watu wanaokadiriwa kufikia milioni moja walifurika katika eneo
maarufu mjini Berlin la sherehe, ambako wanamuziki wa kundi la Pet Shop Boys
walitumbuiza na dakika 11 za kurusha fashifashi angani zilikuwa kivutio
kikubwa.
Mitaa kuelekea lango kuu la Brandenburg ilikuwa imefurika watu
na ilikuwa ni vigumu mtu kuweza kupita kirahisi hata katika saa kabla ya sherehe
hizo. Majira ya usiku wa manane , fashifashi 6,000 zilirushwa angani zikisikika
kwa sauti kishindo kikubwa na rangi mbali mbali za kupendeza.
Jiji hilo
la Berlin lilisikika sauti za kuripuriwa kwa fashifasi mchana
kutwa.
Mwaka waanza Australia
Mwaka ulianzia mjini Sydney , ambako
zaidi ya watu milioni moja waliokuwa wakijiburudisha walijazana katika bandari
ya mji huo kwa ajili ya kuona tukio maarufu la onyesho la kurushwa kwa
fashifashi ambalo linakamilisha sherehe za kuukaribisha mwaka mpya na kisha
kusogea upande wa magharibi kuifunika dunia yote.
Fashifashi katika
bandari ya mji wa Sydney.
Watu waliotembelea mji
huo mkubwa nchini Australia waliburudishwa na miripuko 100,000 ya fashifashi
kutokana na tani saba za fashifashi zilizowekwa katika daraja na matishari
bandarini hapo.
Mwanamuziki nyota wa muziki wa pop, Kylie Minogue
aliongoza hesabu ya dakika za mwisho kuelekea mwaka mpya akiliongoza kundi la
watu waliokuwapo katika eneo hilo ambapo watayarishaji wa sherehe hizo wanasema
zinaweza kuzidi zile zinazofanyika kila mwaka mjini New York , mjini London na
Berlin.
Mwanamuziki Kylie
Minogue akitumbuiza.
Nchini Ufilipino ,
mahospitali yaliwekwa katika hali ya tahadhari wakati maafisa wakitoa miito ya
dakika za mwisho ya kuachana na taratibu za kawaida za kufyatua fashifashi na
kufyatua risasi hewani.
Wafilipino wafukuza bahati mbaya ya mwaka
jana
Wafilipino kwa kawaida hufanya kelele nyingi, ikiwa ni pamoja na
ufyatuaji wa fashifashi, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwa imani
kuwa wanaifukuza bahati mbaya ya mwaka uliopita na kuvutia bahati nzuri katika
mwaka mpya. Baadhi ya watu wanaosherehekea hufyatua risasi hewani.
Vinywaji wakati wa
kuukaribisha mwaka mpya 2013.
Nchini Japan , ambako
watu wengi wamegeukia dini kutokana na nchi hiyo kutumbukia katika mdororo wa
uchumi mwaka jana wa 2012, watu wameanza kufurika katika maeneo ya ibada kusali
wakiomba ufanisi na afya njema.
kiasi ya watu milioni 100 wanatarajiwa
kutembelea maeneo ya ibada katika muda wa siku tatu zijazo.
Mwaka mpya wa 2013
umekaribishwa kwa aina yake duniani kote,wakati mamilioni ya watu wakimiminika
katika bandari ya mjini Sydney nchini Australia,eneo la sherehe mjini Berlin na
mjini London kuangalia fashifashi.
Pia kulikuwa na tukio lililozoeleka la kuweka tufe la dunia katika uwanja wa Times mjini New York , sherehe ambazo zilichafuliwa na kifo mwaka jana cha Dirk Clark , mshauri maalum wa muziki wa rock ambaye kwa miaka kadha amekuwa akisimamia sherehe hizo katika televisheni moja ya Marekani licha ya kuathirika na ulemavu uliosababishwa na ugonjwa wa kiharusi.
Fashifashi zikirushwa
angani kuukaribisha mwaka mpya mjini Berlin.
Mjini Berlin , mamia kwa maelfu ya watu waliokuwa wakifurahia waliunganisha mikono yao katika mitaa iliyojaa watu katika juhudi zao za kutaka kuvunja rekodi ya dunia kwa kucheza midundo ya muziki maarufu wa Gangnam style, uliopigwa na mwanamuziki kutoka Korea ya kusini kwa muziki wa kufoka foka Psy. Gangnam , na wachezaji hao walicheza kwa kufuatia mirindimo ya kuhesabu dakika kuelekea mwaka mpya.
Watu wanaokadiriwa kufikia milioni moja walifurika katika eneo maarufu mjini Berlin la sherehe, ambako wanamuziki wa kundi la Pet Shop Boys walitumbuiza na dakika 11 za kurusha fashifashi angani zilikuwa kivutio kikubwa.
Mitaa kuelekea lango kuu la Brandenburg ilikuwa imefurika watu na ilikuwa ni vigumu mtu kuweza kupita kirahisi hata katika saa kabla ya sherehe hizo. Majira ya usiku wa manane , fashifashi 6,000 zilirushwa angani zikisikika kwa sauti kishindo kikubwa na rangi mbali mbali za kupendeza.
Jiji hilo la Berlin lilisikika sauti za kuripuriwa kwa fashifasi mchana kutwa.
Mwaka waanza Australia
Mwaka ulianzia mjini Sydney , ambako zaidi ya watu milioni moja waliokuwa wakijiburudisha walijazana katika bandari ya mji huo kwa ajili ya kuona tukio maarufu la onyesho la kurushwa kwa fashifashi ambalo linakamilisha sherehe za kuukaribisha mwaka mpya na kisha kusogea upande wa magharibi kuifunika dunia yote.
Fashifashi katika
bandari ya mji wa Sydney.
Mwanamuziki nyota wa muziki wa pop, Kylie Minogue aliongoza hesabu ya dakika za mwisho kuelekea mwaka mpya akiliongoza kundi la watu waliokuwapo katika eneo hilo ambapo watayarishaji wa sherehe hizo wanasema zinaweza kuzidi zile zinazofanyika kila mwaka mjini New York , mjini London na Berlin.
Mwanamuziki Kylie
Minogue akitumbuiza.
Wafilipino wafukuza bahati mbaya ya mwaka jana
Wafilipino kwa kawaida hufanya kelele nyingi, ikiwa ni pamoja na ufyatuaji wa fashifashi, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwa imani kuwa wanaifukuza bahati mbaya ya mwaka uliopita na kuvutia bahati nzuri katika mwaka mpya. Baadhi ya watu wanaosherehekea hufyatua risasi hewani.
Vinywaji wakati wa
kuukaribisha mwaka mpya 2013.
kiasi ya watu milioni 100 wanatarajiwa kutembelea maeneo ya ibada katika muda wa siku tatu zijazo.
Post a Comment