Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FREEMASONS NA HEKA HEKA ZA MWISHO WA DUNIA


Naam!  Disemba 21, 2012 imepita; Sayari yetu haikugongwa na kupasuka na Hatukuona mwisho wa dunia! Lakini ni nini kimetokea? Ilifanyika mikutano kadhaa katika pande nne za dunia. Moja ya mikutano hiyo ni ule uliofanyika Vatican siku 18 (6+6+6) kabla ya Disemba 21. Mkutano huo ulifanyika siku ya Disemba 3, 2012 ukiwahusisha wakuu wa kanisa Katoliki katika kile kinachojulikana kama ‘Pontifical Council for Justice and Peace’ ambapo kiongozi mkuu wa kanisa hilo Papa Benedict xvi ndiye aliyehutubia mkutano huo. Akihutubia makumi ya makadinali waliohudhuria kwenye mkutano huo Papa Benedict xvi alitoa wito wa kuundwa kwa serikali ya dunia (world government)  itakayokuwa na mfumo mpya wa dunia (New world Order) kwa ajili ya kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi. Kiongozi huyo wa kanisa alikaririwa akisema kwamba kuna umuhimu wa kuundwa kile alichokiita: “construction of a world community, with a corresponding authority,”  Kisha akaongeza kusema:The proposed body (World Government) would not be a superpower, concentrated in the hands of a few, which would dominate all peoples, exploiting the weakest. Maneno hayo yanamaanisha kuundwa kwa chombo cha dunia kitakachokuwa na mamlaka ya umma ambacho hakitakuwa chini ya watu wachache watakaowanyonya wanyonge. Itakumbukwa kwamba mwaka 2010 Papa Benedict xvi alitoa wito wa kuundwa kwa ‘Central World Bank’ itakayoshughulikia maswala ya fedha duniani kote.

Sasa msikilize muumini wa freemason na mfanyabiashara za kibenki bwana Paul Warburg akisema kwamba "We will have a world government whether you like it or not. The only question is whether that government will be achieved by conquest or consent." (maneno hayo aliyasema siku ya February 17, 1950, alipokuwa akilihutubia baraza la Seneti nchini Marekani).Warburg alimaanisha kwamba serikali ya dunia lazima ianzishwe, utake au usitake. Swali ni kama serikali hiyo itaanzishwa kwa makubaliano au kwa vita.

Mwaka 1992, Dr. John Coleman aliandika kitabu kinachoitwa ‘Conspirators Hierarchy: The Story of the Committee of 300’. Katika kitabu hicho Dr. Coleman anaainisha watu wanaohusika na mchakato mzima wa kuundwa kwa serikali moja ya dunia au New World Order. Katika ukurasa wa 161 Dr. Coleman anaelezea malengo ya kamati ya watu 300 (mwenyekiti wake akiwa ni mkuu wa kanisa duniani) na kusema:"A One World Government and one-unit monetary system, under permanent non-elected hereditary oligarchists who self-select from among their numbers in the form of a feudal system as it was in the Middle Ages. In this One World entity, population will be limited by restrictions on the number of children per family, diseases, wars, famines, until 1 billion people who are useful to the ruling class, in areas which will be strictly and clearly defined, remain as the total world population.

There will be no middle class, only rulers and the servants. All laws will be uniform under a legal system of world courts practicing the same unified code of  laws, backed up by a One World Government police force and a One World unified military to enforce laws in all former countries where no national boundaries shall exist. The system will be on the basis of a welfare state; those who are obedient and subservient to the One World Government will be rewarded with the means to live; those who are rebellious will simply be starved to death or be declared outlaws, thus a target for anyone who wishes to kill them. Privately owned firearms or weapons of any kind will be prohibited."

Kwa ufupi maneno hayo yanamaanisha kwamba kutakuwepo na serikali moja na mfumo mmoja wa kifedha ambapo kiongozi wa serikali hiyo atachaguliwa na watu 300 wanaounda kamati kuu ya serikali hiyo. Idadi ya watu duniani itapunguzwa kwa kuanzishwa sharia za kuwa na idadi maalumu ya watoto katika familia ambapo mbinu itakayotumika kutekeleza lengo hilo ni kusababisha magonjwa, vita, njaa hadi idadi ya watu ifikie bilioni moja duniani kote. Kutaanzishwa mfumo mmoja wa kijeshi utakaosimamia sharia katika nchi zote ambapo mipaka yote ya nchi zote itaondolewa. Wale watakaokuwa watiifu katika serikali hiyo watawezeshwa kuishi; wale watakaokuwa wapinzani na waasi wataanchwa wafe kwa njaa au kuhumiwa kama wavunja sharia. Haki ya kumiliki silaha za aina yoyote itaondolewa’. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni watoto 20 na waalimu wao 6 waliuawa kwa kupigwa risasi katika shule moja huko Marekani. Baada ya tukio hilo serikali ya Marekani imeanza kupitia upya sheria za umiliki wa silaha kwa watu binafsi.

Rais Barack Obama aliyeshinda uchaguzi ulioshirikisha vyama 6 nchini Marekani amekwisha saini mabadiliko kadhaa ya sheria. Rais Obama amesaini sheria inayoitwa TARP (Troubled Asset Relief Program) ambapo chini ya sheria hiyo mabenki yote (Wall street) pamoja na mabenki ya kigeni yanakuwa katika dhamana kwa serikali. Sheria nyingine ni H.R 347 (House Resolution) au “Federal Restricted Buildings and Grounds Improvement Act of 2011,”. Sheria hii inazuia maandamano ya kwenda kwenye majengo ya serikali ikiwa ni pamoja na zuio la kuendeleza majengo na ardhi. Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Marekani (American Civil Liberties Union –ACLU)) wanaipinga vikali sheria hiyo kwamba inawagandamiza wanyonge. Sheria nyingine ni‘National Defense Authorization Act’ – NDAA. Sheria hii inampa nguvu na mamlaka rais wa Marekani kuamuru kukamatwa na kufungwa gerezani kwa mtu yeyote bila hata ya kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka. Kama ulikuwa unafikiri kwamba rais Morsi Mohamed wa Muslim Brotherhood Misri amejipatia madaraka makubwa kupita kiasi, basi yupo pia rais wa Marekani chini ya NDAA!

Najua wengi watanishangaa ninaposema kwamba uchaguzi wa rais Marekani ulishirikisha vyama 6 na sio viwili. Ili usiniulize maswali juu ya hilo, vyama hivyo ni: 1)Democratic –Baraka Obama; 2)Republican – Miti Romney; 3)Libertarian Party - Gary Johnson; 4) Green Party - Jill Stein; 5) Constitution Party - Virgil Goode; na 6) Justice Party - Rocky Anderson.Kwa nini vyama 6 – ni namba ya utawala wa freemason.Kwa nini vyama vingine havikusikika? Ni kwa sababu Illuminati ndio walioshikilia ‘media’ na wao ndio waamuzi wa nani atangazwe na nani hapana.

Nini maana ya wito wa kuundwa kwa ‘world community’ pamoja na ‘Central World Bank’ kutoka kwa Papa Benedict xvi? Ni kutimizwa kwa unabii wa Ufunuo 13:17. Haitawezekana kuzuiwa kuuza na kununua kama hakuna chombo kinachosimamia uchumi na fedha. Chombo hicho ni ‘Central World Bank’ (CWB). Lakini pia CWB haitakuwa na nguvu za kusimamia shughuli za kifedha kama hakuna serikali nyuma yake. Serikali hiyo ni ‘World Community Authority’ au ‘World Government’ yaani serikali ya dunia.

Wakati Papa Benedict xvi akitoa wito wa kuleta ‘haki na amani’ duniani, chuo kikuu cha Kiislamu (Sunn Al - Azhar University) kimetoa shukrani kwa Vatican kutokana na juhudi za kanisa Katoliki kwa kukemea vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani duniani, kutetea imani za watu wote pamoja na kuziwezesha dini zote kutumia alama na nembo kama utambulisho wa dini husika.

Akihojiwa na waandishi wa habari, Mahmoud Azab ambaye ni mshauri wa Sheikh anayesimamia kitengo cha mahusiano ya kidini (interfaith Dialogue) katika chuo kikuu cha Al-Azhar, aliwashukuru wote wanaotetea ukweli na heshima ya dini. Mahmoud Azab alikuwa akijibu hotuba iliyotolewa hapo kabla na msemaji wa Vatican Fr. Federico Lombardi.  Kwa nini Mahmoud atoe shukrani kwa Papa kutokana na matumizi ya alama/nembo katika dini? Unaweza kuchunguza alama/nembo kwenye jengo la chuo kikuu cha Al-Azhar na jengo alipokaa Papa Benedict xvi akihutubia baraza la haki na amani Vatican. Unazikumbuka kanuni 3 wanazotumia freemasons kufanya kazi zao? Tafakari!

Itakumbukwa kwamba baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Benghazi na kuuawa kwa aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya kutokana na hasira za waumini wa kiislamu zilizotokana na kutolewa kwa sinema inayomkashifu SAW Mohammad (Innocence of Muslims), Fr. Federico Lombardi  alitoa matamko na kusema kwamba: “profound respect for the beliefs, texts, outstanding figures and symbols of the various religions is an essential precondition for the peaceful coexistence of peoples”akiwa anamaanisha kwamba ili pawepo na amani kwa watu, kunatakiwa pawepo na kuheshimu imani, maandiko pamoja na alama/nembo mbalimbali zinazotumiwa na dini kama utambulisho wao. 

Akielezea kwa nini pamekuwepo na mjadala kati ya Al-Azhar University na Vatican, Abdel Muti al-Bayoumi, mjumbe wa ‘Islamic Research Academy’ katika chuo kikuu cha Al-Azhar alisema kwamba mjadala huo hauhusiani na kauli ya Papa Benedict xvi aliyoitoa kwa kuwatetea Wakristo wa dhehebu la Christian Copts wa Misri ambao wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na kushambuliwa kwa sababu ya imani yao. Alipoulizwa kutoa kauli juu ya mjadala kati ya pande hizo mbili, Mahamoud Azab alisema, ““I have nothing to say on the subject at this present time” akimaanisha kwamba hawezi kusema juu ya mjadala huo kwa wakati huu. Hata hivyo Azab alikemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya waumini kwa kuchoma Biblia wakati wa maandamano yaliyofanyika kupinga sinema ya ‘Innocence of Muslims’. Aliwataka waislamu wote kuheshimu Torah, Injili na maandiko Matakatifu kwa sababu ndivyo alivyofanya mtume Mohammad SAW.

Safari ijayo tutaendelea na mada yetu ya heka heka za Freemasons kuelekea mwisho wa Dunia na tutaangalia Kwa nini pawepo na mfululizo wa mijadala kati ya Al-Azhar University na Vatican; serikali ya Iran na Vatican na hata serikali ya Saud Arabia na Vatican?
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top