HALI ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini si ya kuridhisha kutokana na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini Msumbiji
Kutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishio Msumbiji wamejitolea kumchangia nauli ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa ndugu zake
Akizungumza jijini Dar es Salaam mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni , Kaftany Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa wa msanii huyo ingawa haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka sasa
Alisema kutokana na hali kuwa mbaya baadhi ya watanzania wameamua kumchangia msanii huyo ili aweze kurejea nyumbani ili taratibu za matibabu zifwatwe
"Ni kweli hali ya msanii mwenzetu si nzuri anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na Dokta hivyo bado hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na juhudi zinazofanywa ili kumrudisha nyumbani " alisema Masoud
Aliongezea kuwa kwa upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo atakapofika hapa nchini
Matumaini ni msanii kwenye upande wa uchekeshaji.alianza kazi hiyo katika kundi la Kaole na kujipatia umaarufu kwa kuigiza na msanii mwenzie Kiwewe
Post a Comment