Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KAMATI ZA BUNGE KUUNDWA UPYA

Kamati za Kudumu za Bunge zilizoundwa katika Bunge la 10, zinamaliza muda wake katika mkutano wa 10 ulioanza jana na zitaundwa upya wakati wowote kabla ya kuahirishwa kwa mkutano huo.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, uhai wa kamati hizo unakoma baada ya miaka miwili na nusu ya Bunge husika.

“Wakati wowote kuanzia sasa Spika (Anna Makinda anaweza kutangaza kamati mpya za Bunge maana zilizopo zimemaliza muda wake,” alisema mmoja wa wakurugenzi wa Bunge.

Alisema kuundwa kwa kamati hizo upya kunalazimika kufanywa wakati huu kwa kuwa kuna baadhi ambazo zinatakiwa kupatiwa kazi ya kufanya na kuwasilisha kwenye Bunge la bajeti ambalo litaanza Aprili mwaka huu.

Alisema wabunge watatangaziwa kuomba kamati wazitakazo kuzifanyia kazi. Hata hivyo, maamuzi ya mwisho ya mbunge yupi awapo kwenye kamati husika linabaki kuwa chini ya Spika wa Bunge.

Spika Makinda katika mkutano wa tisa, alikaririwa akisema kuwa Bunge litaunda Kamati ya Nishati na Madini mpya ambayo aliiivunja kutokana na sakata la baadhi ya wabunge kutuhumiwa kuhongwa na kampuni za mafuta.

CHANZO: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top