Taarifa ikufikie kwamba
Waziri mkuu Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara
kwa kuwaeleza kuwa kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa kijijini Madimba
mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa
viwanda, hii ikiwa ni kauli tofauti na ya madai ya wakazi hao ambao hasira zao
zilichangiwa na taarifa kwamba kiwanda hicho kingejengwa Dar es
salaam.
Kwenye mkutano wa
majumuisho uliofanyika january 29 2013 Waziri mkuu baada ya kusikiliza madai ya
wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, amesema hakuna tone la gesi ghafi
itakayosafirishwa kwa njia ya bomba.
Namkariri akisema “Imani
yangu ni kwamba maelezo yametosheleza, mtakua na kiwanda chenu cha kusindika,
mtakua na kiwanda cha kusafisha, mtakua na hayo matawi kadhaa kwa ajili ya
uzalishaji wa umeme kwa ajili ya usindikaji wa
viwanda”
Mwanzoni madai ya wakazi wa
Mtwara yalikua ni kupinga usafirishaji wa gesi ghafi mpaka Dar es salaam
wakieleza kwamba huo mpango utafukuza wawekezaji wa viwanda Mtwara ambao
ungechochewa na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa
gesi.
Kwenye mstari mwingine Waziri Mkuu aliwataka wananchi kumsamehe mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia kwa kauli alizotoa december 21 2012 katika kikao cha kamati ya ushauri pale alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo december 27 ambapo aliwaita wapuuzi na wahaini.Pia wananchi walipinga ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kinyerezi Dar es salaam na badala yake wakataka hiyo mitambo ijengwe hukohuko Mtwara.
Waziri mkuu katika
majumuisho yake aliambatana na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya kazi
profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri wa
elimu na mafunzo ya ufundi stadi Dr. Shukuru Kawambwa na Waziri wa mambo ya
ndani Dr. Emmanuel Nchimbi.
Katika hizo siku mbili pia
Waziri mkuu alikutana na vyama vya siasa vya upinzani, chama cha Mapinduzi CCM,
viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo, Wafanyabiashara, Madiwani na wenyeviti
wa mitaa pamoja na
Wanaharakati.
Post a Comment