Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kituo cha huduma ya Afya cha Aga Khan chazindua Mradi wa kuboresha Afya ya mama na mtoto Morogoro

Mratibu wa Mpango wa kuboresha afya ya mama na mtoto, (JHI) wa Aga Khan, Sisawo Konteh, akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa afya ya mama na mtoto kwa Mkoa wa Morogoro. Mradi utakao wezesha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa mama na mtoto, Pamoja nae ( Katikati) Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo, na Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Elias Mtandu.
Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Elias Mtandu (Kushoto), akiwa pamoja na Meya wa manispaa ya Morogoro Amir Nondo (Kulia) na Mratibu wa mradi wa afya ya mama na mtoto wa Aga Khana Sisawo Konteh (Kushoto) , wakinyanyua mikono ikiwa ni ishara ya kushikana mikono pamoja  katika kuunga mpango wa huduma bora ya Afya ya mama na Mtoto kwa Mkoa wa Morogoro.
Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo akifungua Shampeni katika uzinduzi wa Mpango wa Afya bora kwa Mama na mtoto kwa Mkoa wa morogoro. Pamoja nae ni Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan Morogoro, Dr Hugo Yeste.
Mratibu wa mpango wa kuboresha afya ya Mama na mtoto ( JHI)  wa Aga Khan, Sisawo Konteh, akizungumza na Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuunga mkono huduma bora za afya kwa mama na mtoto kwa mkoa wa morogoro 
--
•        Ni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
•        Mradi umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Canada
•        Hii ni kulingana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia 4 na 5
 
Morogoro, Januari 2, 2013 – Kituo cha Huduma za Afya cha AKHS kimezindua mradi ambao utachangia kuboresha huduma ya afya ya  mama mjamzito na mtoto nchini Tanzania uzinduzi uliofanyika mkoani morogoro.
 
Mradi huo unaojulikana kama Tushikane Mikono Kuboresha huduma kwa Wajawazito, na Afya ya Mtoto (Joining Hands: Improving Maternal, Newborn and Child Health (JHI), umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Canada (CIDA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania.
 
Mradi huo wa JHI ni kulingana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs 4 na 5, ambao umelenga kuchangia kuboresha uzazi kwa wajawazito na watoto wachanga, (MNCH) katika mikoa mitano ya Tanzania.
 
Mradi huo utatekelezwa kupitia Kituo cha Huduma ya Afya cha Aga Khan nchini Tanzania (AKHST) na vituo vyake vitano vya afya ya awali (PMCs) kwenye mikoa ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, na Morogoro ikiwa na lengo la kujenga uwezo wa huduma za Afya kwa jamii na kuimaimarisha uhusiano na huduma ngazi ya rufaa.
 
Aidha, Mradio huo wa JHI unajivunia Shirika la Kimataifa la CIDA juu ya uwekezaji mkubwa nchini Tanzania na mtazamo wake juu ya nia yake ya kipaumbele kwenye sekta ya afya nchini.
 
Mradi huo pia utatumika kwa kuinua uwekezaji mkubwa uliofanywa na CIDA pamoja na serikali katika kutekeleza mikakati yake.
 
Malengo ya mradi huo wa JHI ni pamoja na: kuboresha ubora wa huduma kwa wajawazito, Afya ya Mtoto na kulenga kuongeza uwezo wa maeneo ya mradi; kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma za Wajawazito, Watoto na Afya ya Mtoto na kulenga watu wa kipato cha chini na makundi ya wakazi maskini, na hasa katika kuongeza uwezo wao wa kupata nafuu wa kupata huduma, ubora wa huduma za Afya ya uzazi na Wajawazito, Watoto na huduma ya Afya kwa mtoto katika ngazi ya kwanza ya vituo vya Afya; na kuboresha njia za afya, usafi na lishe ya familia kwa walengwa husika (MNCH) kuongeza mahitaji ya huduma (MNCH) ubora kwa walengwa; na kuongeza maarifa uhamisho na kubadilishana juu ya masuala muhimu katika Ushirikiano MNCH Umma muktadha (PPP).
 
Mradi wa JHI wa kuboresha  Afya ya mama na mtoto ulizinduliwa Julai 2012 nchini Tanzania na unatarajiwa kuendelea hadi mwaka 2015.

Mwisho …
 
Mhina Shabani.
Media Executive GDCC
0764 61 54 81
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top