Hayo yalielezwa na daktari bingwa wa uchunguzi wa
magonjwa katika Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk
Henry Mwakyoma na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa.
Madaktari hao wametaja mambo mengine yanayoweza
kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kuwa ni kujiingiza kwenye mapenzi
katika umri mdogo, kuolewa mara nyingi, kuwa na wapenzi wengi, kusafisha sehemu
za siri kwa bidhaa zenye kemikali na kuzaa mara nyingi.
Katika kiwango cha kimataifa, wastani wa mwanamke kuzaa
bila kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa saratani, ni watoto
wanne.
Dk
Mwakyoma alisema saratani ya shingo ya kizazi inatokana na aina 40 ya virusi,
aina mbili ikiwa ni virusi vinavyosambaa kwa njia ya ngono... “Human papilloma
virus (HPV) Squamos cell carcinoma kirusi namba 16 na Adenocarcinoma namba 18,
ni kati ya virusi 40 vinavyosababisha saratani ya kizazi na vyenyewe vinachangia
tatizo hilo kwa asilimia 70.”
Alisema saratani ya uzazi ndiyo inayoongoza
ikilinganishwa na nyingine nchini na asilimia 80 ya wagonjwa, wameambukizwa kwa
ngono.
“Saratani hiyo husambaa kwa ngono kutoka mwanamke mmoja
kwenda kwa mwingine. Mwanamke mwenye saratani ya kizazi akifanya ngono,
mwanamume huchukua virusi na kumwambukiza mwingine atakayefanya naye ngono,”
alisema na kuongeza:
“Wagonjwa wengi na wale ambao tayari wana maambukizi,
wamekuwa wakikutwa na virusi hawa wa aina mbili ambao wamekuwa wakienezwa zaidi
kwa njia ya zinaa. Inawezekana mwanamume akawa ametoa kirusi kwa mwanamke mmoja
kwenda kwa mwingine.”
“Hata hivyo, kuna wanaume ambao tayari wameshakuwa na
maambukizi ya HPV wanatembea na virusi, hawa tunawaita (high risk sexual male
patner) wanaume hawa utakuta kila akioa mke anakufa kwa saratani ya shingo ya
uzazi, lakini kamwe virusi hao hawawezi kumwathiri yeye.”
Alisema kuanza ngono mapema nako kunachangia kwa kiasi
kikubwa maambukizi ya saratani hiyo, kwani binti anakuwa katika hatari zaidi ya
kupata maambukizi mapema na hivyo kuweza kumwathiri mapema zaidi, tofauti na
yule aliyeanza baadaye.
“Idadi kubwa ya wanawake wamekutwa na saratani mapema
sana, ukilinganisha na umri wao, lakini wengi wao wamekuwa wakikutwa na ugonjwa
huu kuanzia umri wa miaka 35 kwenda juu. Hii inamaanisha kuwa walipata
maambukizi hayo walipokuwa na miaka 20-25.”
Dk
Mwakyoma alisema licha ya hivyo mgonjwa anaweza asitambue tatizo hilo mpaka
miaka 10 hadi 15 baadaye ambapo tatizo linajitokeza
hadharani.
“Unapopata maambukizi ya HPV inakuchukua muda mpaka
kujulikana, kwa kawaida mwanamke anaishi miaka 10 hadi 15 na baadaye
anagundulika na tatizo hili, lakini itategemea na kushuka kwa kinga
zake.
Kama ikitokea hapo katikati ukajitokeza ugonjwa mwingine
kama HIV basi saratani nayo itajitokeza.”
Alisema utafiti walioufanywa Septemba 2011 kuhusu tatizo
la HIV na saratani ya shingo ya uzazi unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake
waliokuwa na maambukizi ya HIV na CD4 ziliposhuka tu, saratani ya kizazi nayo
iliibuka, hiyo inamaanisha kuwa tatizo hilo ni kubwa tofauti na
linavyodhaniwa.
Dk
Kahesa kwa upande wake alisema virusi vya HPV huambukizwa kwa mwanamke moja hadi
mwingine, pale mwanamume anapofanya tendo hilo na mwanamke mwenye maambukizi na
kwenda kufanya tendo hilo na mwanamke mwingine.
Kinga
Madaktari hao wameeleza kinga ya maradhi hayo kuwa ni pamoja na matumizi ya kondomu na uaminifu wa wapenzi katika uhusiano wao.
Madaktari hao wameeleza kinga ya maradhi hayo kuwa ni pamoja na matumizi ya kondomu na uaminifu wa wapenzi katika uhusiano wao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk
Seif Rashid alitoa wito kwa Watanzania kujijengea tabia ya kupima mara kwa mara
ili kubaini maambukizi mapema.
Alisema ongezeko la watu wanaougua saratani ya shingo ya
uzazi imetokana na ongezeko kubwa la watu, ikiwa ni pamoja na tabia ya kuchangia
ngono kwa wapenzi.
Alisema chanjo ya saratani ya shingo ya uzazi
inayotarajiwa kuanza kutolewa kwa mabinti wa miaka tisa mpaka 12 baadaye mwaka
huu, ni moja ya juhudi ya Serikali katika kupambana na ugonjwa
huo
-Mwananchi leo
Post a Comment