KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imekataa hesabu za
Halmashauri ya Wilaya ya Geita, baada ya kubainika ubadhirifu wa fedha za miradi
ya maendeleo zaidi ya sh bilioni 4.648.
Fedha zinazoelezwa kuliwa ni pamoja na zile za miradi ya ujenzi wa barabara, stendi ya basi, maji, kilimo, afya ya msingi na maendeleo ya kilimo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Iddi Azzan, alisema ufisadi huo ambao utachunguzwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni wa fedha za bajeti ya mwaka 2010/2011 za halmashauri hiyo.
Azzan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni (CCM), alisema kutokana na ubadhirifu huo wajumbe wa kamati yake wameazimia uanzishwe uchunguzi wa kina kabla ya kuwachukilia hatua viongozi wa halmashauri hiyo.
“Kutokana na madudu hayo, kamati imeiagiza ofisi ya CAG kwa kushirikiana na Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la Polisi kuchunguzi kwa kina fedha zilizotumika ili tujiridhishe na kuchukua hatua zaidi za kisheria,” alisema Azzan. Mhe. Iddi Azzan
Alisema katika hesabu hizo walibaini kuna ujenzi wa stendi ya mabasi ya wilaya hiyo ambao umegharimu kiasi cha sh milioni 500 kutokana na kiwanja chake kutokuwa cha bei hiyo.
Pamoja na stendi, alisema pia kuna ujenzi na ukarabati wa barabara ambao umegharimu sh milioni 748; kwamba kiasi cha sh bilioni 1.5 ambazo zilitolewa kwa ajili ya mfuko wa afya pia kuna sh bilioni 1.9 kwa miradi mingine ya maendeleo ambazo zimetumika isivyo.
“Hatukuridhishwa na mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo hasa za ujenzi wa barabara na stendi kwa matofali ya kuchoma ambayo yameanza kuharibika… vivyo hivyo miradi mingine imeashiria kuna ufisadi ndani yake na ndio maana tunahitaji ukaguzi,” alisema.

Chanzo: Tanzania Daima
Post a Comment