PICHA ZA GARI LA MZEE
LILILOPATA AJALI. DEREVA ANAITWA YANGA ANASTAHILI SIFA ZA PEKEE KWA KWELI
ALIFANYA KAZI KUBWA KUMKWEPESHA MZEE NA AJALI MBAYA KABISA
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa amenusurika kifo, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la bwawani mkoani morogoro.
Gari hilo la Mh. Lowassa liligongwa na basi la morobest, wakati basi hilo lilipolipita basi jingine kwenye daraja na kukutana uso kwa uso na gari la Mhe. Lowassa, Lakini dereva wa mzee kwa ustadi mkubwa alilikwepesha gari lisigonge upande alipokuwa amekaa mzee na kuligonga ubavuni nyuma kwa upande wa dereva. hakuna aliyejeruhiwa.Lowassa na msafara wake aliendelea na safafri hadi morogoro ambako ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Kilakala..
Aizungumzia ajali hiyo, Lowassa amesema mkono wa Mungu ni mkubwa, bila ya hivyo simulizi zingekuwa nyingine juu yake. Pia alisema kuwa wakati alipoliona basi likiwa linakuja upande wake kuwagonga, ukamjia wimbo mmoja wa dini unaonesema kuwa ''hivi haya yote ya nini, ni huruma tu''.

Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa mpaka.Gari ya waziri mkuu mstaafu
ndiyo iliyoharibika kwa kuvunjika vioo.
Post a Comment