Mwenyekiti wa Kamati ya
Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akiwapongeza
makamanda wa vikosi vilivyoshiriki sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu
wakati wa hafla ya kupongezana iliyoandaliwa na Makamanda wa vikosi hivyo juzi
usiku katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani, mjini
Zanzibar.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar, Mama Asha Suleiman Iddi, akimtunza mtanashati Maryam Juma, katika
wimbo wake wa kusifu mapinduzi ya Zanzibar
kutimia miaka 49 kwenye tafrija ya kupongezana makamanda baada ya kumaliza
gwaride la shereh hizo Januari 12 mwaka huu.
Uzalendo
ulimshinda Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd, na kuamua
kujumuika na Kikundi cha Utamaduni cha Diamond Modern cha JKU kwenye tafrija ya
makamanda kupongezana baada ya kumaliza kuchapa gwaride uwanja wa
amani.
Baadhi
ya Makamanda wa Vikosi
vya ulinzi na usalama wakitafakari sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu
wakiwa kwenye tafrija ya kupongeza Bwawani Mjini
Zanzibar.
Ilikuwa
ni siku ya furaha kwa makamanda wa Vikosi vya ulinzi na usalama wakipongezana
baada ya kazi nzito ya kuchapa gwaride Januari 12 mwaka huu wa 2013. Picha Zote
na Hassan wa Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Zanzibar
**************************
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujiandaa mapema na maandalizi makubwa ya
maadhimisho ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia miaka 50
sawa na Nusu karne ambazo zitatarajiwa kuwa za
Kihistoria.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar ambae pia ni Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitoa kauli hiyo wakati wa tafrija
maalum ya kupongezana na kuelewana kwa Maafisa wa Gwaride iliyofanyika katika
Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif
alisema ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali lazima kila Mashirika, taasisi,
Jamii na hata watu binafsi wanapaswa kuanza na maandalizi mapema kwa lengo la
kupata ufanisi unaokusudiwa.
Amesema
Serikali itaendelea kuunga mkono Vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuwa ndivyo
vinavyonafasi kubwa ya kusherehesha vyema katika kilele cha sherehe hizo za
mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi Seif
alieleza kwamba Vikosi vya ulinzi na usalama vimefanya kazi mwaka huu
iliyopelekea kufurahisha na kupendeza miongoni mwa wananchi walioshuhudia
maadhimisho hayo.
“ Lazima
niungame kwamba sherehe za mwaka huu zilikuwa za aina yake hata baadhi ya
wajumbe walioshuhudia maandalizi ya mwisho ya gwaride hilo walipendekeza baadhi
ya askari kutunzwa kutokana na ukakamavu waliouonyesha”. Balozi Seif
aliwapongeza maafandi hao kwa kazi nzito
walioifanya.
Alifahamisha
kwamba Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yameleta faida kubwa
kwa wananchi waliowengi na kuwafanya kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya
kusherehekea sherehe hizo.
Akimkaribisha
Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe na maadhimisho ya Taifa Balozi Seif, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohd Aboud Mohd alisema
majeshi ya ulinzi yameonyesha umahiri mkubwa katika kuchapa
gwaride.
Mh. Aboud
Alieleza kwamba Serikali inajivunia kazi kubwa inayotekelezwa na majeshi ya
ulinzi na usalama Nchini hasa wakati jamii inapokumbwa na majanga na kupelekea
maafa.
Mapema
Kamanda wa Brigedi 101 Zanzibar ambae ndie mkuu wa Gwaride hilo Bridedia General
Sharif Sheikh ameahidi kwamba Vikosi vya ulinzi na usalama vitaendelea
kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuona maandalizi ya
maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50 yanafanikiwa
vyema.
Brigedia
General Sharif Sheikh alieleza matumaini yake kwamba sherehe zijazo zitakuwa za
aina yake zinazotarajiwa kuwa za kistoria ndani ya Visiwa vya Zanzibar na
Tanzania kwa Ujumla.
Tafrija ya
Makamanda na maafisa hao wa Vikosi vya ulinzi na usalama imekuja baada ya kazi
kubwa na ngumu iliyofanywa ba Vikosi vyua ulinzi na usalama katika kufanikisha
gwaride la maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi zilizochukuwa takriban siku
30.
Burdani
safi iliyokuwa ikitolewa na Kikundi cha Diamond Modern Taarab kutoka Jeshi la
Kujenga Uchumi Zanzibar { JKU } ilianikiza ndani ya ukumbi huo wa Bwawani hasa
pale ulipoimbwa wimbo wa mafanikio ya Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 50
chini ya mwimbaji Mtanashati Maryam Juma.
Othman Khamis
Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/1/2013.
Post a Comment