Waziri wa Fedha Dkt.
William Mgimwa (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya tathmini ya mapitio ya mwenendo wa
uchumi wa Tanzania iliyofanywa na Shirika la fedha duniani(IMF) . Wengini ni
Mwakilishi Mkazi wa IMF Thomas Baunsgaard(kulia) na Naibu Waziri wa Fedha Janet
Mbene(kushoto). Picha na Shakila Galus-MAELEZO-Dar es salaam
**************
Shirika la Fedha
Duniani(IMF) limepoingeza Tanzania kwa usimamizi mzuri wa kisera ambao umesaidia
utulivu wa kiuchumi ambao umesaidia kuleta matumaini hatua iliyosababisha
mfumuko wa uchumi hapa nchini kuendelea kushuka.
Kauli hiyo imetolewa leo
na Mwakilishi Mkazi nchini wa IMF Thomas Baunsgaard wakati wa mkutano wake yeye
na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa na waandishi wa habari jijini Dar es
salam juu ya kuelezea tathmini ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania
iliyofanywa na Shirika la fedha duniani(IMF) .
Alisema kuwa ni muhumu
kuendelea kudhibiti sera za mapato na matumizi ya serikali na sera za usimamizi
wa fedha ili kuwa na uchumi endelevu.
Bw. Baunsgaard alisema
kuwa Tanzania imedhamiria kuchukua hatua za ziada ili kuhakikisha inafikiwa
lengo la kupunguza mfumuko wa bei hapa nchini.
Aidha alisema kuwa Bodi ya
utendaji wa shirika la IMF imeidhinisha nyongeza ya dola za Kimarekani 57 na
kuifanya Tanzania kuweza kunufaika na mkopo wenye masharti nafuu toka IMF
unaofikia dola za kimarekani 114.
Vilevile Bodi iliridhia
ombi la Serikali ya Tanzania la kupewa msamaha wa kukuika kigezo cha madeni ya
nje yenye masharti ya kibiashara kwa sababu ukiukaji huo hauwezi kuathiri
uhimilivu wa deni la Taifa.
Post a Comment