Baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum
(Chadema), Regia Mtema, Estaratus Mtemanyenza
akitoa shukrani wakati wa kumbukumbu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu
kifo cha mbunge huyo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Naibu
Waziri wa Sheria na Katiba, Angella Kairuki.
Katibu wa Kamati
ya Maandalizi na Msemaji wa Regia Foundation, Olivia Sanare akizungumza wakati
wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum
(Chadema), Regia Mtema. habari kwa hsiani ya http://francisdande.blogspot.com/
DAR ES
SALAAM, Tanzania
ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia
Mtema, ametimiza mwaka mmoja tangu kufariki kwake, ambapo Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, alihudhuria maadhimisho
hayo na kusema demokrasia ya kweli haigaiwi katika sahani ya dhahabu, bali kwa
kuipigania.
Makamba alienda mbali zaidi na kuongeza kuwa,
wanaopaswa kupigania haki hiyo ni vijana ambao wanayo nafasi kubwa katika safari
ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka
2015.
Makamba alitoa kauli hiyo jana usiku katika hafla
ya kumbukumbu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Regia, aliyefariki kwa
ajali ya gari Januari 14, mwaka jana - hafla iliyofanyiola katika Hoteli ya
Peacock jijini Dar es Salaam.
Akitoa mada iliyohusu vijana na namna
anavyomfahamu Regia, Makamba alisema kama vijana watatumika vizuri katika
demokrasia, watakuwa chachu ya maendeleo na kwamba ujana peke yake si sifa ya
kuwa kiongozi.
Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM),
alisema lazima uchaguzi wa mwaka 2015 uamuliwe na vijana kama alivyokuwa na
uthubutu wa kufanya mambo makubwa Regia.
Naibu waziri huyo aliwataka vijana kutafakari ni
kwa nini walijiandikisha kwa wingi bila ya kwenda kupiga kura katika chaguzi
mbili za 2005 na 2010 na kwamba uchaguzi ujao ni lazima wabadilike na kufanya
uamuzi mgumu.
Alitoa mfano kwamba, mwaka 2015, watajiandikisha
vijana wapya milioni 5 na kutimiza zaidi ya waliojiandikisha milioni 25,
uchaguzi utakuwa umetendewa haki na vijana.
Hata hivyo alisema ili kusukuma gurudumu la
maendeleo si lazima vijana wakagombea uongozi katika siasa tu bali hata katika
sekta na shughuli zingine.
“Sikugombea nafasi ya uongozi katika nchi hii
kwa sababu ya kutaka ukubwa, bali nilifanya hivyo ili vijana waige kutoka kwangu
na kama sasa wengine walivyoiga kwa Regia,” alisema
Makamba
Akizungumzia alivyomfahamu Regia, Makamba alisema
alimfahamu siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka
2010, katika midahalo iliyokuwa ikirushwa na televisheni
nchini.
“Nikiwa naangalia mdahalo wabunge waliokwenda
kugombea majimboni, nilimwona Zitto, Halima na dada mwingine ambaye sikumfahamu
akiwa nao, naye akizungumza namna anavyokwenda jimboni huku akitoa maelezo
mazuri,” alisema Makamba
Makamba alisema baadae alifahamiana zaidi kwa
kuonana na kushirikiana naye katika mambo mbalimbali bungeni ambapo alikiri
Regia alikuwa ni mtu mwenye uwezo na upeo mkubwa wa
mambo.
Post a Comment