Katibu wa TFF, Angetile Osiah kulia akizungumzia wagombea waliowekewa pingamizi. Kushoto ni Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura. |
Na Mahmoud
Zubeiry wa Bin Zubeiry
WAGOMBEA
wote wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya
Ligi Kuu, wamewekewa pingamizi wasigombee uongozi kwa sababu
mbalimbali.
Katibu Mkuu
wa TFF, Angetile Osiah ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF,
amewaambia Waandishi wa Habari mchana huu katika ukumbi wa Mikutano wa TFF,
uliopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kwamba, jumla ya pingamizi 14 zimewafikia
tangu Jumatatu wiki hii hadi zoezi hilo linafungwa jana.
Angetile
aliwataja wagombea waliowekewa pingamizi kuwa ni Jamal Malinzi, Athumani
Nyamlani wanaogombea Urais wa TFF, nafasi inayoachwa wazi na Leodegar Tenga
anayeng’atuka, Michael Wambura anayegombea Umakamu, nafasi inayoachwa wazi na
Nyamlani anayehamia kwenye Urais.
Angetile
alisema kwamba kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu, wagombea wa Uenyekiti Yussuf
Manji, Ahmad Yahya Juma na Mgombea Umakamu, Mohamed Said pia wamewekewa
pingamizi.
Aidha,
wagombea wa nafasi za Ujumbe, Epatha Swai, Eliud Mvella na Athumani Kambi nao
wamewekewa pingamizi.
Nyamlani
amewekewa pingamizi mbili, moja na Mtanga Yussuf Gacha na nyingine ya Menard
Justinian, wakati Malinzi amewekewa pingamizi moja na Agape Fuwe na Wambura ana
pingamizi mbili, moja ya Osiah Samuel Msengi na nyingine ya Saidi
Rubeya.
Epatha Swai
amewekwa pingamizi na Ramadhan Sesso na Sos Chalamila, Eliud Mvella amepingwa na
Saidi Kiponza, Abdul Changawa na Peter Namengi, wakati Athumani Kambi amepingwa
na Jeremiah John Wambura
Wakati Manji
amewekewa pingamizi mbili, na mwanachama maarufu wa Simba, Daniel Tumaini Kamna
na mwanachama wa Yanga, Juma Ally Magoma, Frank Mchaki amewawekea pingamizi
Ahamd Yahya na Mohamed Said.
Angetile
amesema Kamati itakutana Jumatano kujadili pingamizi hizo na amewakumbusha wote
waliowekewa pingamizi kufika ofisi za TFF saa 4:00 asubuhi siku hiyo kusikiliza
pingamizi zao.
Post a Comment