Marubani
wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya ukaguzi wa
mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es Salaam leo
asubuhi. Hii ni baada ya wahandisi wa shirika hilo kukamilisha kufunga
kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani. Ndege hii aina
ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilisitisha safari
zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele katika chumba cha marubani kupata
ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya
ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake
za kawaida, imeanza tena safari za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
Kapteni
Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa
mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8
Q300 .Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22. Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.
Post a Comment