Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MBARONI KWA KUSAFIRISHA BINADAMU

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linawashikilia raia wawili wa kigeni na Mtanzania mmoja kwa tuhuma za kufanya biashara za kusafirisha binadamu na raia wengine wanne wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinononi, Charles Kenyela, alisema jana kuwa watu hao walikamatwa Januari 9 mwaka huu, majira ya saa 5:00 usiku, eneo la Kimara Bonyokwa nyumbani kwa Issa Omar (39) ambaye ni raia wa Tanzania.
Alisema watu hao walikamatwa baada ya raia wema kutoa taarifa polisi kwamba kulikuwa na raia wa kigeni wasiofahamika ambao wamehifadhiwa kwenye nyumba ya mkazi huyo.
Hata hivyo, alisema mwenye nyumba hiyo alitoroka baada ya kutambua kuwepo kwa polisi katika makazi yake.
Alisema katika upekuzi huo, watu wanne raia wa Ethiopia walipatikana wakiwa wamefungiwa kwenye chumba kimoja ndani ya nyumba hiyo.
Aliwataja watu hao kuwa ni Maarufu Abdulhman (23), Tasfahun Larebo (23), Sesibo Handore (20) na Solomon Wathiro (20).
Kamanda Kenyela alisema kuwa baada ya kukamatwa Omari, Januari 10 mwaka huu, mkazi huyo alieleza kuwapo kwa wahusika wakuu wa biashara ya kusafirisha binadamu.
Alisema Omari aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ndayishimye Abdulkabir (30), mfanyabiashara, mkazi wa Msave Kayanzi na Nuwayezi Blaise (24), mwanafunzi wa Chuo cha Bridge, wote raia wa Burundi.
Alisema watu hao walikamatwa katika Hoteli ya Lunch Time iliyoko Manzese na kwamba walipohojiwa walikiri kuwa kweli wao ni raia wa Burundi, walipopekuliwa walikutwa na hati za kusafiria zenye namba OP 0024157 na OP 0004268 zilizotolewa mwaka 2012 pia walikuwa na kadi za ATM za Benki ya ABSA na FNB.

Chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top