DCI ROBERT MANUMBA.
UKWELI
kuhusu hali ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba,
utajulikana leo wakati akiendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu wa wauguzi na
madaktari wa Hospitali ya Aga Khan.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, aliyekuwapo hospitalini hapo, alisema hadi sasa wanasubiri kauli ya daktari wake na kisha watajua la kufanya.
Alisema hivi sasa hawawezi kuchukua uamuzi wa aina yoyote hadi pale madaktari watakapotoa mapendekezo yao ya kitaalamu.
“Bado anaendelea na matibabu na yupo chini ya ungalizi maalumu lakini kwa sasa tunasubiri uamuzi wa madaktari wake wanaomtibia ambao watatoa tamko lao kesho (leo), hivyo ninaomba tuvute subira katika kipindi hiki.
“Siwezi kusema jambo lolote kwa sasa lakini ridhika na hatua hii niliyokuambia kwa sasa ndio maana tupo hapa hospitali kwa lengo la kufuatilia kila hatua juu ya hali ya afya na matibabu ya DCI Manumba,” alisema Senso.
MTANZANIA ilimshuhudia mmoja wa ndugu wa karibu wa DCI Manumba, akiwaambia wenzake hivi sasa hali imebadilika tofauti na ilivyokuwa awali.
“Kuna mabadiliko ya mgonjwa, nimeingia ndani muda si mrefu na ukimgusa hivi sasa anashituka na tunamshukuru Mungu ikiwa ataendelea hivi hivi,” alisikika ndugu huyo akimwambia mwenzake.
Juzi, Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Aga Khan, Dk. Jaffer Dharsee, alisema DCI Manumba bado yupo chini ya uangalizi katika chumba cha wagonjwa walio katika uangalizi maalumu (ICU) na anahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi.
“Kama tunavyofahamu kuwa DCI Manumba ni kiongozi mkubwa hivyo umma wa Watanzania unapenda kufahamu hali yake.
Sisi bado tunaye hapa hospitali akiwa chini ya uangalizi mkubwa wa madaktari na wauguzi kwa sababu afya yake inahitaji uangalizi wa karibu.
“Anaendelea kupatiwa matibabu na tunaamini dawa anazopatiwa zitaweza kumsaidia kwa matibabu na tunafanya kila linalowezekana.
Hivyo tutaendelea kupeana taarifa na nitakapokuwa tayari nitawajulisha zaidi,” alisema Dk. Dharsee.

Post a Comment