Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI YUSUPH MWENDA AZINDUA UJENZI WA DARAJA LA NDUMBWI, MBEZI JUU, DSM

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yusuph Mwenda alifanya ziara ya uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Ndumbwi, Kata ya Mbezi Juu mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam. Daraja hilo linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 211 na kampuni ya ujenzi ya genimex Construction Ltd litasaidia kuondoa kero ya muda mrefu ya wakazi wa Kata ya Mbezi Juu kufuatia kukatika kwa mawasiliano baina ya wakazi hao kutokana na mvua za mara kwa mara zilizokuwa zikinyesha. Aidha, ujenzi wa Daraja jingine lilaounganisha wakazi wa Ndumbwi na Zahanati utaanza hivi karibuni. Pichani ni sehemu ya ziara yake pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo.

Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Gerald Urio (wa pili kushoto) akimpa maelezo Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda (wa tatu kulia) aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa Manispaa hiyo, Serikali za Mitaa na vyama vya siasa, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Ndumbwi, Mbezi Juu, Dar es Salaam wakati wa ziara ya Meya ya uzinduzi wa ujenzi huo mwishoni mwa wiki. Daraja hilo linajengwa kwa gharama ya shilingi milioni 211.

Mstahiki meya, Yusuph Mwenda pamoja na viongozi mbalimbali wa Kata, Serikali ya Mtaa na wa vyama vya siasa wakikagua ujenzi wa daraja hilo
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ndumbwi, Mbezi Juu, Salustian Kimario (kulia) akimpa maelezo Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kulia) aliyeambatana na viongozi mbalimbali wa Manispaa hiyo na vyama vya siasa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto ndumbwi, Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam wakati Meya huyo alipofanya ziara ya uzinduzi wa ujenzi huo, mwishoni mwa wiki
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Mbezi Juu mara baada ya uzinduzi wa Daraja la Ndumbwi. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Mbezi Juu, Alhaj Issa Mwinyimbegu na Diwani wa Kata ya Hanansif, Abbas Tarimba.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Mbezi Juu wakifuatilia kwa makini
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top