Kaimu
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel
Nderumaki akiogea na viongozi wa PPF Pensheni Fund wakati walipotembelea
TSN kufahamiana na kujifunza mambo mbalimbali katika makutano ya
barabara za Nelson Mandela na Nyerere Dar es Salaam jana. Kutoka
(kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, Mkurugenzi wa
Mipango na Uwekezaji Bw.Steven Alfred,Meneja wa Kanda, Mbaruku Magawa na
Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
Msanifu
kurasa wa gazeti la HabariLeo, Ephraim Mwaluvinga (kulia) akiwaonesha
jinsi maadalizi ya gazeti yanavyofanywa kwa ugeni kutoka PPF
ulipotembelea chumba habari cha gazeti hilo Dar es Salaam jana.
Mhariri wa Magazeti ya wikiendi ya DailyNews, Ichikaeli Maro akiukaribisha uongozi wa PPF ulipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo. Katikati ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki.
Mhariri wa Magazeti ya wikiendi ya DailyNews, Ichikaeli Maro akiukaribisha uongozi wa PPF ulipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo. Katikati ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki.
Fundi
Mitambo wa TSN, Rashid Singandole, akieleza jinsi mitambo ya uchapaji ya
Standard Printers inayomilikiwa na TSN inavyofanya kazi, kwa uongozi wa
PPF uliotembelea kiwanda hicho. Kuanzia kushoto ni Kaimu Mhariri
Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William
Erio, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji,Steven Alfred, na Meneja
Uhusiano wa Mfuko huo,Bi. Lulu Mengele.
Kaimu
Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki (kulia) akiueleza jambo ugeni
wa PPF baada ya kutembelea mitambo ya kampuni hiyo muda mchache kabla
ya kuondoka.
Post a Comment