Mkuu wa
Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa
Na Rahimu
Kambi, Kilindi
Mganga
Mkuu wa Zahanati ya Kata ya Saunyi, Tarafa ya Mgela, wilayani Kilindi mkoani
Tanga, Rashid Mhande, anasakwa na porisi baada ya kufumwa akiiba dawa zenye
thamani ya zaidi ya Sh Milioni tano.
Tukio
hilo lilitokea juzi, baada ya Mhande kufumwa akiiba dawa kwa kutumia toroli la
Zahanati hiyo, kabla ya kuzihamishia kwenye pikipiki yake kwa ajili ya
kuzipeleka anakojua yeye.
Akizungumza
jana usiku, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, mkoani Tanga, Selemani Liwowa, alisema
kwamba hadi sasa mganga huyo hajulikani alipo, huku akiagiza asakwe popote alipo
ili afikishwe kwenye vyombo vya dola.
Alisema
hospitali hiyo imekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakisema mara
kadhaa wanaambiwa hakuna dawa, jambo linalowapa wasiwasi mkubwa.
“Tunashukuru
kubainika kwa mganga huyo aliyekuwa anaiba dawa katika zahanati ya Saunyi, jambo
ambalo hakika limetusikitisha mno kwa watumishi kama hawa.
“Baada ya
kubainika, baadhi ya wananchi walianza kumpiga, hivyo kufanikiwa kukimbia,
ambapo alipofika polisi alisingizia amepigwa na wafugaji, hivyo kupewa matibabu
Makao Makuu ya wilaya, hata hivyo alipoona atagundulika janja yake kutoka kwa
wananchi na serikali, aliamua kutoroka kusipojulikana," alisema
Liwowa.
Kwa
mujibu wa Liwowa, ameagiza porisi wamsake mhalifu huyo ili sheria zichukuwe
mkondo wake kwa watumishi wanaohujumu Taifa na kuiletea aibu serikali kwa
vitendo vyao visivyokuwa vya kiungwana.
Post a Comment