![]() |
| Kikosi cha Miembeni |
Na Mahmoud
Zubeiry, Zanzibar
TIMU ya
Coastal Union ya Tanga imetolewa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, baada
ya sare ya bila kufungana na Miembani FC jioni hii kwenye Uwanja wa Mao Dze
Tung, Zanzibar.
Matokeo hayo
yanaifanya Miembeni isubiri hatima yake ya kuingia Nusu Fainali katika mchezo wa
usiku wa leo kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
ya kumaliza mechi zake tatu ikiwa katika nafasi ya pili, nyuma ya Azam
inayoongoza Kundi A kwa pointi nne pia na wastani mzuri wa
mabao.
Timu tatu
sasa zina nafasi ya kuingia Nusu Fainali, Miembeni yenye pointi nne sawa na Azam
na Mtibwa Sugar ambayo ikiwa na pointi moja hivi sasa, ikishinda usiku itatimiza
pointi nne na mustakabali wake wa kusonga mbele utatazamwa kutokana na wastani
wake wa mabao.
Tayari
kutoka Kundi A, mabingwa wa Kenya, Tusker FC wamefuzu kama vinara wa kundi hilo,
wakati Simba SC, mabingwa wa Bara wamefuzu kama washindi wa
pili.
Mshindi wa
kwanza wa Kundi A atamenyana na mshindi wa pili wa Kundi B katika Nusu Fainali,
wakati mshindi wa kwanza wa Kundi B atamenyana na mshindi wa pili wa Kundi
A.



Post a Comment