Marehemu Anthon Simbaulanga
************
MPIGANAJI
wa Vita vya pili vya Dunia, Mzee Anthon Simbaulanga, amefariki Dunia jana,
Januari 15, katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga, huku
akihisiwa na kuwa na miaka isiyopungua 120.
Mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Magunga, iliyopo wilayani Korogwe
mkoani Tanga, huku akitarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya kijiji cha
Komsala.
Habari
zilizoifikia Handeni Kwetu na kuthibitishwa na mtoto wa marehemu, Paulina
Anthon Simbaulanga, zilisema mwili wa baba yao utazikwa kesho baada ya ndugu
kuungana kwenye msiba huo mzito katika familia yao.
“Kwa sasa
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Magunga kwa ajili ya
kusubiri ndugu waliokuwa sehemu mbalimbali kuwasili kwa maziko yake,” alisema.
Mzee
Simbaulanga, alipofanya mazungumzo na Handeni Kwetu mwishoni mwa mwaka jana,
alionyeshwa kukerwa na kunyimwa haki yake ya mafao baada ya kupigana vita vya
pili vya Dunia.
Habari za
mafao yake zilifika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, wilayani Muhingo
Rweyemamu na kuagiza kukutana na mwakilishi wa mzee huyo ili azungumze naye na
kujua cha kufanya, ukizingatia kuwa ndio kwanza ameingia katika wilaya hiyo,
baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwaka jana.
Post a Comment