RAIS wa Jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 31/12/2012 ametangaza rasmi matoke
ya takwimu ya sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2012, ambapo idadi ya
watanzania imeonekana kuongezeka kwa asilimia kubwa zaidi ya vipindi vinne vya
sensa tokea sensa ya kwanza kufanyika mwaka 1967 hadi leo ikiwa ni sensa
ya tano kufanyika.
Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na
Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania
wote walikuwa ni Milioni 12, 313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11,
958,654 na Visiwani Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo,
Sensa kama hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012,
ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002 ambapo Tanzania Bara wapo Watu 43,625,434 na Tanzania Zanzibar idadi yao ni 1,303,568.
MSIKILIZE RAIS KIKWETE AKITANGAZA MATOKEO YA SENSA.
.
MSIKILIZE RAIS KIKWETE AKITANGAZA MATOKEO YA SENSA.
.
Post a Comment