Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA AWAANDALIA HAFLA YA CHAKULA CHA MCHANA MAMALISHE NA WAMACHINGA WA JIJI LA MWANZA

 

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (katikati) akiwa ameambatana na Mzee Masalakulangwa (kulia) na Bw. Alfred Wambura ambaye ni mlezi wa Shirika la wamachinga Mwanza (SHIUMA) wakiingia ukumbi wa New Mwanza Hotel kushiriki hafla ya chakula cha pamoja na Mamalishe na Wamachinga wa Mwanza, iliyoandaliwa na Mstahiki Meya .

Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula.
"Tumejumuika hapa leo ili kufahamiana zaidi kuweka mikakati na malengo kwa mwaka mpya 2013 lakini pia kuhakikisha kero na matatizo mbalimbali yanayojitokeza ndani ya shughuli zetu na jamii yanashughulikiwa na viongozi wa Serikali ngazi zote husika.." By Mstahiki Meya.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na Mamalishe pamoja na wamachinga waliojitokeza jana kushiriki hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula.

Bw. Alfred Wambura ambaye ni mlezi wa Shirika la wamachinga Mwanza (SHIUMA) akitambulisha viongozi wa vitengo mbalimbali ndani ya Shirika la Wamachinga ambalo linajumuisha Mamalishe, Madreva wa pikipiki na Madereva wa Taxi, kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mstahiki Meya ndani ya ukumbi wa New Mwanza Hotel.

Mwenyekiti wa madereva wa pikipiki jijini Mwanza Bw. Makoye akiainisha kwa ufupi majukumu wali yoazimia kuyafanikisha kwa msimu wa Mwaka 2013 wakiwa sehemu ya wamachinga walioshiriki hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mstahiki Meya ndani ya ukumbi wa New Mwanza Hotel.

Sehemu ya kusanyiko la wamachinga na hawa ni madereva wa Taxi.

Sehemu ya wamachinga waliojitokeza ukumbi wa New Mwanza Hotel kushiriki hafla ya chakula cha pamoja na Mstahiki Meya

Wakisikiliza kwa umakiiini yaliyojiri kabla ya chakula cha pamoja.

Of coz yenye kufurahisha nayo yalikuwepo.

Wamachinga kusanyikoni.

Kisha wamachinga hao wakashiriki chakula cha pamoja.

Kwautaratibu maalum wamachinga walijongea kwenye meza za 'menyu'.

Tukio hili lililoandaliwa na mstahiki meya kwa wadau hawa, upande wao walilitumia pia kama sehemu ya sherehe yao ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top