Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo akisalimiana na wana CCM wakati akiingia ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala tayari kwa Mkutano wa ndani na viongozi wa CCM wa wilaya ya Temeke huku akipokelewa kwa shangwe na viongozi hao.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo akiwafunda viongozi wa Temeke kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Dar Live. Pia alipokea kero zinazoisibu CCM kwa wilaya ya Temeke
Vijana nao hawakuwa nyuma kumsikiliza kwa umakini mkubwa Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo kama wanavyoonekana pichani.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo akiondoka ndani ya ukumbi wa Dar Live . Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema
Mjumbe wa Baraza kuu la Wazazi Taifa, William Malecela akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John wakati wa kutoka Dar Live.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo akienda kufungua shina jipya laWakereketwa la Wafanyabiashara wa Rangi Tatu
Wafanyabiashara Mbalimbali wa Rangi Tatu wakifurahia uzinduzi wa shina la Wakereketwa la Rangi Tatu lenye zaidi ya watu 200 mara baada ya Bendera ya CCM ya Shina hilo kupandishwa juu na Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo akisoma kilichoandikwa kwenye Shina hilo. Kushoto kwake ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John akishuhudia tukio hilo.
Hitimisho la Ziara ya Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo ilikuwa ni kwenye Mkutano wa Hadhara ambapo alianza kwa kuwapokea wanachama wapya zaidi ya 800 waliojiunga na CCM hii leo.
Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Ndg Abdallah Bullembo (katikati), Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Ndg Anjela Kiziga (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema wakiwasalimia Wananchi waliohudhulia Mkutano huo wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Zakheim Mbagala
Loading...
Home » Unlabelled » MWENYEKITI WA WAZAZI TAIFA WA CCM, NDG ABDALLAH BULEMBO AFANYA ZIARA YA KIHISTORIA WILAYA YA TEMEKE, MBAGALA
Post a Comment