Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu hoja
mbalimbali zilizoibuliwa na jopo la APRM kuhusu Demokrasia na Utawala Bora
nchini Tanzania. Mhe. Rais alitoa ufafanuzi huo mbele ya Mkutano wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa,
Ethiopia.
Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora.
Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Demokrasia na Utawala Bora
nchini Tanzania. Wengine katika picha ni Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili
kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwemo pia wajumbe
na Wabunge waliofuatana na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano
huo.
Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe aliofuatana
nao nchini Ethiopia ambao unajumuisha Mawaziri, Wabunge na Timu ya APRM,
Tanzania
Post a Comment