Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS KIKWETE: TUNAAJIRI WAALIMU 28,000

SERIKALI imesema itaajiri na kusambaza walimu 28,746 katika shule za msingi na sekondari kuanzia Januari mwaka huu.
Hatua hiyo ilitangazwa juzi na Rais Jakaya Kikwete wakati akiwa mjini Igunga, akisema hatua hiyo itasaidia kupunguza ukosefu wa walimu katika shule za serikali nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Kikwete, alisema kuwa walimu 14,600 watakuwa wa shule za msingi, huku 14,060 wakiwa wa shule za sekondari na 80 wa vyuo vya ualimu.
Alisema kuwa hadi sasa kuna upungufu wa walimu 57,177 katika shule za serikali, tatizo ambalo litamalizika kwa miaka michache ijayo kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya walimu wanaofundishwa katika vyuo mbalimbali nchini.
Rais Kikwete, alisema kuwa mikoa yenye uhaba mkubwa zaidi wa walimu itapewa kipaumbele katika mgawo huo.
Alisema mkoa huo wa Tabora ni moja ya mikoa yenye uhaba mkubwa wa walimu, ikiwa na ukosefu wa walimu 2, 055 na wilaya ya Igunga pekee ikiwa na uhitaji wa walimu 285.
“Mwaka juzi, serikali iliajiri na kusambaza walimu 24,621 ambao kati yao 11,379 walikuwa wa shule za msingi, walimu 13,246 walikuwa wa shule za sekondari na walimu 42 walikuwa ni wa vyuo vya elimu,” alisema.
Rais Kikwete alisema kuwa serikali inakabiliana na matatizo ya sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maabara, ukosefu wa nyumba za kutosha za walimu na ukosefu wa vitabu vya wanafunzi.

Chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top