Rais Barack Obama akizungumza kwenye kikao na waandishi.
RAIS Barack Obama anasema Marekani ilitoa usaidizi mdogo wa kiufundi
kwa operesheni ya uokozi iliyoshindikana ya jeshi la Ufaransa la kuokoa
raia wa nchi hiyo aliyetekwa Somalia.
Katika barua iliyoandikwa na White House kwa viongozi wa bunge na kutolewa Jumapili imesema ndege za kijeshi za Marekani ziliingia kwa muda mfupi kwenye anga ya Somalia katika kutoa msaada kwenye operesheni hiyo ya Ufaransa.
Rais anasema majeshi ya Marekani na ndege za kijeshi hazikuhusika moja kwa moja na shambulizi katika eneo ambalo raia huyo wa Ufaransa alikuwa akishikiliwa.
Maafisa wa Ufaransa wanasema mtaalam wa kijeshi Dennis Alex aliuwawa na watekaji wake wa Alshabab wakati wa juhudi za uokozi katika mji wa Boulmarer kiasi cha kilometa 110 kusini mwa Mogadishu Lakini Al shabab wanasema Allex yu hai na salama.
Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa aliuwawa katika operesheni hiyo na mmoja hajulikani alipo.
Wapiganaji 17 wa Somalia pia waliuwawa.
Post a Comment