KATIBU Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema hatalumbana wala kupigana vijembe tena na wapinzani kwa kuwa ana majukumu makubwa ya kusimamia kero za wananchi.
Amesema badala yake malumbano na vijembe atamwachia kiboko yao Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nauye.
“Kazi hii namwacha Nape yeye ni kiboko yao na anawamudu kwa kuwa anawafahamu vizuri kuliko mimi, ”alisema Kinana.
Kinana alisema Watanzania wana matatizo mengi yanayo hitaji kutatatuliwa na kwamba malumbano pekee hayajengi. Wapinzani nguvu kubwa wanaelekeza kwenye vijembe sisi tunachapa kazi,”alisema.
Alisema sekretarieti hiyo imekwenda Kigoma kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM kwa kutumia treni la TRL.
Kinana aliitaka Serikali kuendelea kulipatia ruzuku shirika hilo ili liendelee kutoa huduma ya usafiri huo ambao ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa kipato cha chini.
Aliwapongeza wafanyakazi wa TRL kwamba wameamua kuchapa kazi badala ya kuzungumza na kwamba ndio maana mafanikio yanaonekana.
Alisema wataalamu wa ndani wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wameonyesha uzalendo mkubwa kufufua reli hiyo.
Alisema wataalamu wa ndani wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wameonyesha uzalendo mkubwa kufufua reli hiyo.
“Tumeamua kuwaunga mkono kwa kusafiri na treni kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma ili kujionea mafanikio na changamoto zilizopo,”alisema.
Kuhusu suala la upungufu wa chakula mkoani Singida Kinana aliahidi kushughulikia tatizo hilo ili kuwapunguzia adha.Kinana alisema hayo baada ya kuelezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai kwamba mkoa huo unakabiliwa na njaa.
“Sasa hivi nawapigia simu viongozi wa Serikali ili walete chakula haraka,”alisema.
Aliwahakikishia wakazi wa mmkoa huo na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali itatoa chakula kwa wenye njaa.
Aliwahakikishia wakazi wa mmkoa huo na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali itatoa chakula kwa wenye njaa.
Naye Katibu wa Halmashauri kuu, Uhusiano wa Kimataifa Dk, Asha-Rose Migiro aliwataka wana CCM kuungana ili kukipatia chama hicho ushindi katika chaguzi zijazo.
Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nauye alisema safari hiyo kwa njia ya reli ni kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment