Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, baada ya kuwasilisha maoni yake kwenye Tume ya Kukusanya maoni, Sefue alisema nafasi ya Rais inapaswa kuwa imara na yenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania wote.
“Asilimia kubwa ya Watanzania, wamekuwa wakipendekeza rais apunguziwe madaraka aliyonayo, jambo ambalo linaweza kuleta hatari mbeleni, suala hili linatupasa kuwa makini.
“Unajua unaweza kupunguza madaraka ya Rais kiasi ambacho kitamfanya ashindwe kutuunganisha na kuliongoza taifa kwa sababu tayari umedhoofisha nafasi yake.
“Tusiwe wepesi wa kutamka maneno bila ya kutafakari hasara na faida zake, tunapaswa kutambua taifa letu lenye miaka 51 ya uhuru bado masikini, kuna mataifa yenye miaka 200 hadi 400, lakini kamwe hayathubutu kumpunguzia Rais madaraka,” alisema.
Source: Mtanzania 16/01/13
Post a Comment