Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
akisisitiza kwa wajumbe wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012
kuhusu serikali kufuatiliaji maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio
za Mwenge mjini Zanzbar.
Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Ali Nassoro Lufunga akizungumza na viongozi na waratibu wa mbio za
Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu maandalizi ya mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2013.Mkoa wa shinyanga ulikuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge
kwa mwaka 2012.
Serikali inaandaa
utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya miradi yote inayozinduliwa wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakua endelevu na
kuwanufaisha wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo
mjini Zanzibar na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati
akitoa tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2012 na maendeleo ya miradi
iliyozinduliwa wakati wa mbio hizo kwenye mkutano wa viongozi na waratibu wa
mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema serikali ina
wajibu wa kufuatilia kwa karibu miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru
2012 katika Halmashauri za wilaya, manispaa na Miji ili kuhakikisha kuwa gharama
kubwa iliyotumika wakati wa uanzishaji na ujenzi wa miradi hiyo inawanufaisha
wananchi kutoka kizazi kimoja hadi kingine ili kutunza hadhi na heshima ya
Mwenge wa Uhuru.
Amesema mbio za Mwenge
wa uhuru zimezindua miradi mingi nchini yenye thamani ya mabilioni ya fedha na
kuongeza kuwa si dhamira ya serikali kuona kuwa mwenge wa uhuru unatumika tu
kuzindua miradi ya maendeleo bali kuhakikisha uendelevu wa miradi
hiyo.
Post a Comment