Gari aina ya Lori Fuso lenye namba za usajili T. 284 AGL ambalo
lilikuwa na shehena aina ya mirungi viroba vipatavyo 173 vyenye jumla ya
uzito wa kilogramu 1800
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus
Sabas akiongea na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Mkoa wa Arusha
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Camirius Wambura aliyeshika madawa ya
kulevya aina ya mirungi nje ya jengo la Makao Makuu ya jeshi hilo
mkoani hapa mara baada ya kukamata shehena hiyo.(Picha na Rashid Nchimbi
wa Polisi Arusha)
…………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wiki moja tu baada ya jeshi la Polisi Mkoani Arusha kukamata lori aina ya Mitsubishi
Canter lililokuwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi, leo tena Jeshi
hilo limekamata shehena nyingine ya madawa ya aina hiyo ambayo ilikuwa
kwenye lori aina ya Fuso lenye namna za usajili T. 284 AGL
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo limetokea leo muda wa saa 12:30 asubuhi eneo la Engarenaibo lililopo wilayani Longido ambapo madawa hayo yalikuwa yanasafirishwa kutoka nchi jirani ya Kenya kuja hapa nchini kupitia mpaka wa Namanga.
Aliongeza kwa kusema kwamba mirungi iliyokamatwa ni jumla ya viroba 173 vyenye uzito wa kilogramu 1800 na mafanikio hayo yalipatikana baada ya jeshi hilo kupata taarifa toka kwa raia wema na mtu mmoja alikamatwa na anaendelea kuhojiwa huku mwingine akifanikiwa kukimbia.
Baadhi ya viroba hivyo vilionekana kuwa na majina ya watu, uzito na mahali, hali inayotafsiriwa kuwa huwa vinagawanywa kwa watu hao mara baada ya kuingizwa mjini hapa.

Kamanda Sabas aliendelea
kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa ushirikiano wao mkubwa na kuwaomba
waendelee kushirikiana na jeshi hilo hali ambayo itasaidia kupunguza
vitendo vya uhalifu.
Pia Kamanda Sabas aliwaonya
wamiliki wa vyombo vya usafiri hasa magari kutokubali vyombo vyao
vitumike katika usafirishaji wa biashara haramu kwani pindi
vinapokamatwa huwa vinakuwa chini ya vyombo vya dola huku kesi
ikiendelea badala ya kuendelea kufanya kazi nyingine za uzalishaji.
Mpaka hivi sasa kwa muda wa wiki moja ndani ya mwezi huu jumla ya magari
mawili yamekamatwa.
Post a Comment