Naomba kuchukua fursa
hii kutoa shukrani za dhati na wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Kikwete na Serikali yake ya awamu ya nne, kwa niaba yangu binafsi na kwa
niaba yaTawi la CCM UK na nina imani kwa niaba ya wana jamii ya Wa-Tanzania
Walioko Nje ya Nchi (Dispora) kwa Ujumla, katika juhudi anazofanya kujumuisha
Dispora Tanzania kwenye kuchangia maendeleao ya Nchi yetu.
Wana-Dispora tulio wengi
tumeshuhudia kwa vitendo
tangu Rais Jakaya
Kikwete na Serikali yake imeingia Madarakani , jitihada na mikakati tofauti na
iliyo wazi ya Serikali Kuu kutafuta mbinu za kudumu ili kushirikiana na
kuwahusisha wana Diaspora, katika kuchangia maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya
Nyumbani, Tanzania.
Nakumbuka Mheshimiwa
Rais Kikwete katika kikao chake cha kwanza na Watanzania waishio Uingereza Mnamo
mwaka wa fedha 2006/2007 pale Churchill Hotel, UK , katika Hotuba yake ambayo
mbali na kutuelezea mafanikio na mikakati mbalimbali iliyopangwa na serikali
yake kwenye utekelezaji wa Sera zake za Serikali ya awamu ya nne, kwa nia ya
kutimiza maazimio ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005 na baadae 2010, vile vile
alituahidi wana-Dispora kuwa atahakikisha yeye Binafsi atafanya jitihada zake
zote kwa kadri ya uwezo wake aliyopewa na Mwenyezi Mungu na Serikali yake
haitusahau na katuacha nyuma Wana-Dispora . Kilichoendelea baada ya Mkutano ule
wana Dispora UK tulishudia thamani yetu kwa Serikali na Taifa letu ,kwani
tumekuwa tukipewa kipaumbele kwa kila Kiongozi Mkuu wakiwemo Mawaziri na Wabunge
wetu tofauti, wanapotembelea Uingereza (na nina imani Nchi nyingine mbalimbali
) mbali na kuwa na ratiba zao ndefu za kikazi, wanapata muda wa kubadilishana
mawazo nasi na tunaona matunda ya mchango wetu yameanza kuonekana ,licha ya
kuwepo changamoto za kawaida zinazokabilika. Hili tunamshukuru sana Rais wetu
kwa kulipa uzito unaostahili na kuonyesha mfano wa Uongozi wake bora na
uliotukuka.
Kwa mara ya kwanza
Tanzania Dispora tumepata sauti na kuthaminiwa kwa wazi kwa Mchango wetu wa
hali na mali tunaorudisha nyumbani ili kuchangia Maendeleo ya Nchi.
Wana-Dispora sasa tunajivunia kupewa na Rais wetu jina la Mkoa . Baada ya
kuanza na dawati la Dispora pale Wizara ya Mambo ya Nje, ili kuweka mfumo wa
kudumu na kutimiza ahadi yake Mheshimiwa Rais mwaka ulipita 2012 aliteua
Mkurugenzi wa Idara ya Dispora. Sasa tuna Idara/Kitengo kizima na si dawati
tena. Kitengo/Idara yenye jukumu la kushughulikia mambo muhimu na tofauti ya
Dispora. Hii ni hatua kubwa sana na ya muhimu na hatutaacha kumshukuru Rais wetu
kwa kuliona na kulitambua hili na kutuletea matunda yake.
Licha ya yote hayo ya
kiutendaji yanayoendelea, na jambo kubwa lililofanya kuandika shukrani hizi za
dhati na za wazi ni kilichotendeka wiki iliyopita kupitia vyombo vya habari na
Blogu za jamii tumeshuhudia tukio la kihistoria pale ambapo Rais Jakaya Kikwete,
Chini ya Ofisi yake Ikulu , wametoa fursa kwa Wa-Tanzania Wataalamu waliopo Nje
na Ndani ya Nchi kupeleka wasifu wao (CV) moja kwa moja Ofisi za Katibu Mkuu
Kiongozi -Ikulu, ili tuweze kupata nafasi za kazi kuchangia moja kwa moja na
kuwa mstari wa mbele kuijenga nchi yetu . Hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu cha
Watanzania (na hususan Wana-Dispora) kuomba serikali kutumia zaidi wataalamu wa
kitanzania na si wa kigeni , na tumefurahi sana kuwa Serikali yetu kwa mara ya
kwanza na kwa uwazi kabisa imetusikiliza kwa hili .
Naomba kutoa wito na
shime kwa WaTanzania wote waliopo nchi mbalimbali duniani , ni wakati umefika
sasa Nchi yetu inatuhitaji na Serikali yetu imetupa nafasi hii adhimu basi na
tujipange na tujitokeze kwa wingi ili tuweze kwenda nyumbani kuchangia maendeleo
ya Tanzania yetu katika nyanja tofauti na kwa kadri ya uwezo wetu na kwa yale
mazuri tuliyojifunza Ughaibuni.
naomba kumalizia kwa
ule usemi usemao kuwa "Asiyemshukuru Binadamu mwenzie basi hata Mwenyezi Mungu
hawezi kumshukuru " na kwa mantiki hiyo, kwa heshima kubwa Naomba kutanguliza
shukrani zangu za dhati kwa mpendwa Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kujitolea kwake na kufanya kazi ngumu mno ya kuliongoza Taifa letu na
nakumuombea kwa Mwenyezi Mungu yeye Binafsi na Viongozi wetu wote afya njema na
hekima za kuweza kupambana na majukumu yao ya kila siku .
Kwa Wana -Dispora
Wenzangu popote pale mlipo Duniani , ngoma iko uwanjani na tuicheze sasa, CV
zinahitajika .........haya mama Harambeeeee
Mugu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania
Umoja Ni Ushindi
.
Kidumu Chama Cha
Mapinduzi.
Mariam
Mungula
Katibu wa CCM -
Uingereza
Post a Comment