IKICHEZESHA
wachezaji wake vijana wanaoinukia vema, Simba SC jioni hii imelala 1-0 mbele ya
Black Leopard ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Bao pekee la
washindi katika mchezo huo, lilifungwa na beki Hassan Isihaka aliyejifunga
katika harakati za kuokoa dakika ya saba tu ya mchezo
huo.
Pamoja na
kufungwa, watoto hao wa Simba SC waliokwenda ziara ya wiki mbili Oman, walicheza
soka maridadi na kuwaburudisha wapenzi wa timu hiyo.
Ushindi huo,
unaitoa mrithi Leopard ambayo awali katika ziara yake ya wiki moja nchini
ilifungwa mechi mbili na Yanga SC, 3-2 Dar es Salaam Jumamosi na 2-1 jana CCM
Kirumba, Mwanza.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Simba kilikuwa; Abuu Hashim, William Weta, Emiry Mgeta,
Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Ramadhani Singano, Ibrahim
Ajid/Haruna Shamte, Marid Kaheza, Rashid Ismail na Miraji Madenge.
Leopard;
Azwindn Maphala, Ermort Azaga, Thulan Ntishgila, Humphey Khoza, Vicent Mabusela,
Tiyana Mabunda, Mongezi Bobe, Mahlatse Maake, Michael Nkambula , Mxolis Ngunede
na Kodney Ramagalela.
credits: Bin Zubeiry
Post a Comment