Tanzania
imesifiwa na kuelezewa kuwa mfano wa kuigwa katika Kilimo kufuatia
mpango na mkakati wake wa Kilimo nchini maarufu Kama Southern
Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT).
Pongezi
hizo zimetolewa leo asubuhi katika kikao maalum kujadili na kuangalia
mtazamo na mbinu mpya za kuboresha na kuimarisha kilimo,
kilichohudhuriwa na viongozi na wadau wa uchumi duniani, wanaohushuria
mkutano wa Uchumi katika mji wa Davos, mkutano ambao pia umehudhuriwa na
Katibu Mkuu aw Umoja SA Mataifa Ban Ki-Moon.
SAGCOT ni
mpango wa serikali wa kuimarisha, kukuza na kuboresha kilimo kiweze kuwa
cha kisasa zaidi Kwa lengo la kuongeza mavuno na Mapato Kwa ajili ya
matumizi ya ndani na nje ya nchi.
Mkutano wa
leo umetoa pongezi Kwa Tanzania Kwa kuanzisha wazo hilo ambalo nchi
zingine barani Afrika zimeuiga na kuanza kuutekeleza katika nchi zao
ambapo nchi zingine pia duniani zimeanza kuuelewa na kuanza kuweka
mikakati ya kuutekeleza na kuutumia mpango huo ili kuleta mapinduzi ya
Kilimo duniani.
Hapa nchini Mikoa 6 imeanza utekelezaji wa mkakati huo katika Mikoa ya
Dar-Es-Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma, tayari mpango huu umeanza pia kutekelezwa katika mkoa mpya wa Katavi.
Post a Comment