Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas
Masaburi akiwasilisha maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam Ijumaa, jan 18, 2013. Kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino
Ramadhani.
Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally saleh akiongea katika mkutano na Uongozi wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliokutana na Tume kuwasilisha maoni yake
kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. Harry Kitillya (mwenye tai nyekundu) akiongea na
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba mara baada ya
Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba (wa sita
kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodiu ya TRA Bw. Bernard Mchomvu (wa nne
kutoka kushoto) mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba
Mpya jijini Dar es Salaam.
Post a Comment