Tume
ya Mabadiliko ya Katiba imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizoandikwa na vyombo
mbalimbali vya habari yakiwemo baadhi ya magazeti ya jana (Alhamisi, Januari 17,
2013) ambazo zinaashiriakuwa
Tume inakataa kupokea baadhi ya maoni yanayowasilishwa kwake na makundi
mbalimbali.
Taarifa
hizo za vyombo vya habari zimetokana na kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Dkt. Ramadhan Mlinga aliyoitoa mara baada ya
taasisi yake kuwasilisha kwa Tume maoni kuhusu Katiba Mpya siku ya Jumatano,
tarehe 16 Januari, 2013 katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo, mara baada ya PPRA kuwasilisha maoni kwa Tume, Wajumbe
wa Tume walisita kupokea maoni ya taasisi hiyo na badala yake kuagiza PPRA
kuandaa maoni tena na kuyawasilisha katika Tume ndani ya wiki mbili kuanzia
tarehe 16 Januari, 2013.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Alhamisi, Januari 17, 2013) kwa vyombo vya
habari na Katibu wa Tume hiyo Ndg. Assaa Rashid, taarifa hizo siyo za kweli na
kuwa Tume yake haina mamlaka ya kisheria ya kukataa kupokea
maoni.
“Tume
inapenda kuwataarifu wananchi, makundi, taasisi na wadau wengine wote kuwa Tume
haijakataa na haina mamlaka ya kisheria ya kukataa kupokea maoni ya mtu,
jumuiya, taasisi au kundi lolote,” alisema Ndg. Assaa katika taarifa yake na
kuongeza:
“Katika mikutano inayoendelea
(na makundi mbalimbali), kabla ya kuhitimisha mkutano husika, Tumehuomba chama cha
siasa, jumuiya, taasisi au mtu aliyewasilisha maoni kutoa ufafanuzi wa hoja
mbalimbali zilizojitokeza katika kikao” alisema na kufafanua kuwa ufafanuzi huu
hutolewa kwa hiari palepale katika mkutano au kwa maandishi baada ya siku kadhaa
ambazo Tume hukubaliana na mtu au kikundi kilichowasilisha maoni.
Akifafanua zaidi Ndg. Assaa
ameseama kuwa mikutano inayoendelea kati ya
Tume na Makundimbalimbali
inafuatia kukamilika kwa mikutano ya kukusanya maoni binafsi ya wananchi tarehe
19 Disemba mwaka jana (2012).
“Kwa
msingi huu, katika mkutano kati ya Tume na PPRA uliofanyika juzi, tarehe 15
Januari, 2013, Tume iliiomba PPRA kuangalia
uwezekano wa kutoa ufafanuzi wa masuala ya ziada ambayo Tume ilitaka kupata
maoni ya kitaalamu kutoka katika taasisi hiyo,” alisema kiongozi
huyo wa Tume na kuongeza kuwa ombi kama hilo pia limetolewa kwa makundi mengine
ambayo yameshakutana na Tume kutoa maoni kuhusu Katiba
Mpya.
Tume
ya Mabadiliko ya Katiba ilianza kazi rasmi tarehe 1 Mei mwaka jana (2012) na
wiki iliyopita ilianza kazi ya kukusanya maoni ya makundi na watu mbalimbali
kuhusu Katiba Mpya. Mikutano hii inatarajiwa kukamilika tarehe 25 mwezi huu
(Januari, 2013).
Post a Comment